BAR YA KWETU PAZURI TABATA YAFUNGWA KWA KUDAIWA KUTOKUKIDHI VIGEZO.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ameagiza kufungwa kwa
ukumbi maarufu wa Starehe ujulikanao kwa jina la Kwetu Pazuri Tabata
kutokana na kushindwa kukidhi vigezo.
akizungumza
na Globu ya jamii mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili
,Kumbi la Moto amesema kuwa wameamua kufunga ukumbi huo mara baada ya
kufanya na ukaguzi na kujiridhisha kuwa haijakidhi vigezo.
"Tumefanya
ukaguzi na kumchukua Meneja wa Bar hiyo na kumfikisha kituo cha Polisi
Ukonga Stakishari kwa ajili ya kufunguliwa mashataka na baadae
kufikishwa mahakamani"amesema Kumbilamoto.
Amesema
kuwa mara baada ya kutoka katika kituo hicho ,alifikishwa kituo cha
Polisi kati na kukubali kulipa faini ya Milioni mbili na kukukiri makosa
ya kufanya kazi ya Night Club bila kuwa na leseni huku akijua kufanya
hivyo ni kinyume cha sheria.
Aidha
tumewaonya juu ya tabia yao ya kupanga viti karibu na barabara jambo
ambalo ni kinyume cha sheria za Tanroads, " hivyo tumeamua tuifunge
mpaka hapo watakapo jipanga upya",Kumbi la Moto amesema
na kuongeza kuwa kwa muda mrefu watu walikuwa wakilalamika juu ya
sehemu hiyo lakini hatua zilikuwa zinachelewa kuchukuliwa, hivyo
nimefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kuamua kuifunga
Bar hiyo.
Aidha
katika ziara hiyo pia amekagua ujenzi wa maabara ya Zahanati ya kata ya
vingunguti ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

No comments