ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA JIJINI ARUSHA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA
MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
|
||
|
|
||
|
|
Mkurugenzi wa Jiji
|
|
|
Simu:
Nukushi:
|
+255 27 2508073/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
|
S. L. P. 3013,
20
Barabara ya Boma,
23101 ARUSHA,
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Tovuti: www.arushacc.go.tz
|
|
|
||
|
|
|
|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. KASSIMU MAJALIWA wakati wa ziara
yake Mkoani hapa atatembelea Jiji la Arusha kuanzia tarehe 01-03/12/2016 na
kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji, kukutana na
wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi wa Jiji la Arusha.
Kupitia ziara hiyo tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea
Kiwanda cha National Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara
ya Friends Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami
kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais
Tamisemi.
Aidha siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu MHE. KASIMU MAJALIWA atakutana na kuzungumza na watumishi pamoja
walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae atakutana na wafanyabiashara
katika Ukumbi huo.
Hata hivyo katika siku ya tatu ya ziara yake MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea na kukagua viwanda vya Lodhia
pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro na baadae atakutana na
wanachi wote kwenye Mkutano wa hadahara utakaofanyika kwenye uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kuanzia saa nane mchana.
IMETOLEWA NA;
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
30 Novemba, 2016
No comments