VITUO WANAMOISHI WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU AMBAVYO HAVIJASAJILIWA KUFUTIWA


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Vituo vinavyolea watoto yatima na ambao wanaishi katika mazingira magumu ,ambavyo havijazingatia utaratibu kisheria juu ya undesheshwaji wa vituo hivyo na ambavyo havijasajiliwa kufutiwa

Akizungumza Afisa Ustawi wa jamii halmashauri ya Arumeru,Restituta Mvungi ,wakati wa kutoa tuzo kwa kituo bora cha kulea watoto kilichofanya vizuri mwaka huu kwa mkoa wa Arusha ,alisema wameamua kuweka msisitizo wa kutaka vituo vyote visajiliwe kutokana na kuwepo kwa vituo vingi ambavyo havina sifa

Alisema vituo vingi vimekuwa vikianzishwa kiholela hivyo kuzidi kupelekea watoto wengi kuendelea kuishi maisha magumu mitaani

Alisema, sifa ambazo zitawezesha vituo kupata usajili ni vile ambavyo vitapitia ustawi wa jamii ,watoto watakao walea watapitia ustawi wa jamii,na kuwa na mazingira bora ikiwemo kutoa huduma bora za kibinadamu kwa watoto wanaowalea

"Unakuta kuna kituo,mazingira yake mabaya sana ,pachafu vitanda vibovu au hakuna,unakuta watoto hawasomi kula tu ni shida halafu tunaita ni kituo si kweli ni lazima tufunge,"alisema Restituta

"Kwamujibu wa sheria mtoto anatakiwa kuwa na kitanda chake na kinakimo chake kinachotakiwa lakini ukifwatilia hili unakuta kuna watoto hawana vitanda nakumbuka kuna kituo tulikuta hivyo na tukafungia,alisema Restituta

Upande wa mmiliki wa kituo cha kulea watoto cha Small Step Compassion ,Juma Kitau amewasisitiza wamiliki wa vyuo kuacha kutumia watoto kama sehemu ya biashara na badala yake wajitoe kulea watoto

"Kuna baadhi ya vituo wanatumia uchafu wa wale watoto kupata wafadhili,mimi nasema si sawa wamiliki wajifunze kuwaboreshea mazingira bora watoto kwakua ni afya kwao,"alisema Juma

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza ,mkurugenzi wa shirika la Foundation for tomorrow Melissa QueyQuep ,alitoa wito kwa serikali kuendelea kutambua uwepo wa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuwasaidia kwakua watoto hao bado wanahitaji msaada katika jamii

Meneja mratibu wa Shirika la Foundation for tomorrow Edwiga Gilbert, alisema vigezo vya tuzo walizotoa ni pamoja na vituo ambavyo vimeweza kujiendesha vyenyewe bila kutegemea wadhamini,ikwemo ubora na usafi wa kituo

Awali alisema mshindi wa kwanza ni kituo cha Neema Village alipata zawadi ya dola 200 pamoja na cheti cha utambulisho, nafasi zingine zikienda kwa kituo cha Amani Children Centre, Stemm na Falcon Children Home ambako wote walipata zawadi ya dola100 pamoja na vyeti

No comments