Trump amteua Rex Tillerson waziri wa mambo ya nje
Rais mteule nchini
Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil,
Rex Tillerson ndiye waziri wa mambo ya nje nchini Marekani.
Bwana Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wanademocrat na baadhi ya warepublican
Trump ajikita kuboresha uchumi Marekani
Trump akana madai kuwa Urusi ilishawishi uchaguzi
Uteuzi huo unahitaji kuthibitishwa na bunge la Senate.
Siku chache zilizopita ilibainika kuwa majasusi nchini Marekani wanaamini kuwa Urusi ilihusika na kushawishi ushindi wa Trump.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani ndiye mwanadiplomasia wa cheo cha juu zaidi ambaye uhusika na sera za kigeni za nchi.
No comments