RC Gambo kukabidhi Pikipiki 200 – Jumamosi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na waendesha boda boda 200(hawapo pichani) watakaopatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba wakati wa kikao na vijana hao kukamilisha taratibu na masuala ya usalama kabla ya kukabidhiwa Pikipiki hizo.
Kijana muendesha boda boda(aliyesimama) akichangia kuhusiana na kiasi gani cha Fedha kirejeshwe kwa siku ili kukamilisha mkopo wa pikipiki watakazopewa. kwa wakati.
Umoja wa waendesha bodaboda Jiji la Arusha (UBOJA) wakiwa katika
Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa
waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.
Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho
kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.
Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa pamoja kwamba watarejesha shilingi za Kitanzania 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki shilingi 49,000 ama kwa Mwezi itakua shilingi 210,000.
Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasiicho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo
Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.
Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya pikipiki hizo na mwakilishi wa Kishen
Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa
alisema Pikipiki hizo zina warantii ya meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye injini katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyoteau kubadilishiwa Pikipiki nyingine
Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo
ufuatao:
Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.
"Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho "alisema Gambo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema pikipiki hizo zitakabidhiwa siku
tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wote mnakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria
No comments