Mahakam kuu Arusha ya tupilia mbali pingamizi la serikali dhidi kesi ya Lema.
Mbunge Godbless Lema akizungumza na mkewe,juzi baada ya mahakama kumalizika ,pembeni yake ni wakili wake Shekh Mfinaga.picha pamoja na habari Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus Arusha.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali ombi la mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
Jaji
Dkt.Modesta Opiyo ambaye mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi
yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi
walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa
mahakamani.
Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shedrack Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha hoja zao katika kiapo na hati ya dharura.
Akizungumza baada ya kukubaliwa na Jaji ,wakili Mfinanga alimtaka Jaji huyo kusikiliza rufaa hiyo kwani kuchelewa siyo sababu ya msingi sana kwa mujibu wa sheria na kunukuu kesi mbalimbali zilizochelewa kukatiwa rufaa kwa siku nyingi na kudai kuwa mahakama ya rufaa ilizikubali na kuzitolea maamuzi.
Mfinanga amesema na kumwomba Jaji kusikiliza rufaa yao kwa sababu ni ya msingi na kamwe haiwezi kuvunja sheria ya makosa ya jinai iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Mawakili wa serikali wakiongozwa na Wakili Mfawidhi Materius Marandu, Hashim Ngole na Elizabert Swai walipinga vikali kukubaliwa kwa rufaa hiyo kwa madai kuwa Jaji Msengi alitupilia mbali na kurudia kuikubali ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za makosa ya Jinai.
Baada ya malumbano hayo yaliyochukuwa zaidi ya masaa 5 Jaji Opiyo alisema kuwa uamuzi wa kuikubali ama kuikataa rufaa hiyo atautoa kesho Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika mahakama hiyo.
Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.

No comments