Kilio cha mbunge Ridhiwani chasikika, RC Ndikilo atoa mwezi mmoja kwa wafugaji
Kutokana
na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa
nchini, mbunge wa Chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali
kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.
Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya
mapigano baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye
vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi, sasa
yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata
wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa
migogoro ya wakulima na wafugaji.
Kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va
dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge Ridhiwani kikapokewa
vyema na Mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30, kwa wafugaji
waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,
“Mlipokuja
hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani
ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa
wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya
wakulima na wafugaji.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa
Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi,
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna
wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha taratibu
hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto
Ruvu kuwanywesha maji.
Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi
kupoteza mazao yao; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa
kitonga, hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo
hilo.
RC Ndikilo katika hatua nyingine
ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo
hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo
hili la kitonga na mkoa wa Pwani, Mkuu wa mkoa alisema.
Kwa mujibu wa
sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe, walidai kuwa wana
Ng’ombe wapatao laki 5, lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi
hicho. “hata kama ukweli ndiyo huo, eneo la kufuga mkoa wa Pwani
linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo
laki 2 na nusu.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa
Pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa
mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa
mifugo katika Bonde la Ufa ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugaji
walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona maji na
majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji
cha Kitoga kata ya Vigwaza
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo
vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima DC Ndikilo amesema ni vyema wafugaji
wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa
amani na upendo.
Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia
nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale
wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria
hakuna aliyejuu.
Alitoa tahadhari kuwa atashughulika
wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye
ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kiburi.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze mara
baada ya kauli ya Mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa Chalinze kutoa
ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo
iliyoingia kinyemela.
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanakijiji
cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima
na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza.
No comments