Tamasha la waandishi wa habari mkoa wa Arusha kufanyika Nyerere Day.

Katibu wa TASWA  mkoani Arusha Mussa Juma


Mwandishi wetu,Arusha

Wanahabari zaidi ya 400 wanatarajia kushiriki katika Tamasha   la vyombo vya habari, Kanda ya kaskazini, litafanyika kuanzia Octobar 14 siku ya kumbukumbu ya mwalimu Julius Nyerere hadi 15 mwaka huu.

Siku ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere kutakuwa na kongamano  kujadili mchango wa hayati baba wa Taifa, katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na michezo na baadaye octobar 15 kutakuwa na michezo  katika uwanja wa General Tyre katika  jiji la Arusha.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka linaandaliwa na Taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa Arusha(TASWA).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa TASWA  mkoa Arusha, Mussa Juma, alisema litashirikisha wanahabari  400 kutoka mikoa ya Arusha,Manyara, Kilimanjaro na Jijini Dar es Salam.

Juma alisema katika kongamano mada mbali mbali zitatolewa na wabobezi katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na michezo na wanahabari watapata fursa kutambua zaidi mchango kwa hayati baba wa Taifa.

"Mwaka huu, tumeamua kuanza la kongamano ili kukumbushana wanahabari masuala mbali mbali ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu"alisema

Akizungumzia maandalizi ya Bonanza, mratibu wa bonanza hilo Andrea Ngobole wanahabari na timu waalikwa watashiriki michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia, riadha, kukimbiza kuku .

"maandalizi yanakwenda vizuri lakini tunaomba wadhamini zaidi kujitokeza ili kufanikisha tamasha na Kongamano la wanahabari mwaka huu"alisema.

Alisema katika michezo timu ambazo tayari zimethibitisha kushiriki ni TASWA Dar es Salaam ambao ndio mabingwa watetezi, timu za Radio Sunrise,timu za vyuo vya Uandishi habari Arusha, Arusha one Radio, Triple A Radio, Radio 5, ORS Radio ya mkoa Manyara na TASWA Arusha.

"tutangaza zawadi hivi karibuni na pia wageni waalikwa kama ambavyo hufanyika kila mwaka"alisema.

No comments