OXFAM YAWAFUNDA WATUMIAJI WA MITANDAO NCHINI

Na.Vero Ignatus ,Dar es salaam

Shirika la Oxfam wameendesha mafunzo ya siku mbili kwa wadau wanaotumia mitandao ya kijamii na wenye ufuasi wa mitando kuhusiana namna ambavyo wanaweza kuisaidi jamii katika kuleta maendeleo.

Mafunzo hayo yaliyopewa  kauli mbiu #ChukuaHatua yamewashirikisha wadau mbalimbali wenye fani tofauti ambao wanatumia  mitandao ya kijamii.

Mratibu Mawasiliano ya digitali Bill Marwa kutoka Oxfam amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Amesema kuwa kazi kubwa ya Shirika hilo ni kuandaa miradi ya kuwawezesha wanawake ,kupunguza umasikini,Utawala bora,Uwazi na Uwajibikaji

Ametanabaisha kuwa waneamua kutoa mafunzo hayo kwa wamiliki na watumiaji ya mitandao ya kijamii kwasababu nguvu kubwa ya mitandao inakuwa kwa kasi hadi sasa inakadiriwa zaidi ya Watanzania  20milioni wanajipatia taarifa mbalimbalimbali.

Mratibu Mawasiliano ya digitali Bill Marwa akiwa anazungumza na wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na wadau mbalimbali wanaotumia mitandao hiyo ,mafunzo hayo yamefanyika katika Hotel ya Regency Park iliyopo Jijini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog

Afisa Uhusiano Kisuma Mapunda akiwa anazunguma na washiriki wa mafunzo hayo katika Hotel ya Regency Park Jijini Dar es salaam.Picha na Vero Ignatus Blog

Baadhi ya washiriki waliohidhuria katika mmafunzo hayo .Picha na Vero Ignatus Blog.





No comments