BURUNDI yahitaji kuungwa mkono kuwaendelea waalimu wa Lugha ya Kiswahili
Mwalimu Nshimimana Dorothee kutoka chuo kikuu cha Burundi ,Kitivo cha sanaa na Sayansi za Jamii,idara ya taaluma za Kiafrika
Burudi inahitaji kuungwa mkono ili kuendeleza waalimu wa lugha ya kiswahili katika shule za msingi,sekondari hadi vyuo vikuu
Hayo yamesemwa na mwalimu Nshimimana Dorothee kutoka chuo kikuu cha Burundi ,Kitivo cha sanaa na Sayansi za Jamii,idara ya taaluma za Kiafrika ambapo amesema kuwa lugha ya kiswahili ni njia ya mawasiliano Afrika ya mashariki hivyo ikitumiwa vizuri inaweza kuliongezea taifa husika pato,pamoja na uchumi kuongezeka zaidi.
Aidha amesema kuwa nchi husika zione kuwa upo umuhimu wa kubadilishana waalimu wa lugha ya kiswahili katika shule za msingi pamoja na zile za sekondari ili wanafunzi waweze kujengwa katika msingi imara ,hata wanapoendelea na elimu ya juu waendelee kuikuza lugha hiyo na kuifanya kuwa lugha ya Afrika.
Hata hivyo bi Nshirimimana ameiomba Kamisheni ya Kiswahili kuongeza jiti
hada katika kuendeleza ,kukuza,kutunza na kusimamia lugha ya kiswahili ili iweze kukua kwa mapana zaidi.
Aidha amesema changamoto kubwa walionayo ya nchini Burundi kuhusiana na kiswahili ni pamoja na waalimu wa kiswahili hawapati nafasi ya kuendelea na shahada ya pili katika nchi za ulaya kwani katika nchi hizo hawana udhamini wa kiswahili,jambo ambalo limepelekea walimu wengi wa lugha hiyo kuacha kufundisha na kujiunga kwenye kozi nyingine.
Kongamano la kamisheni ya kiswahili lilifanyika septemba 6 mwaka huu kisiwani Zanzibar ,ambapo viongozi wa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki wameamua kuanzisha kamisheni hiyo sambamba na kujitolea kutoa fedha kila mwaka kwa kutambua kwamba kiswahili ni msingi muhimu katika ufanisi wa nguzo nne za utengamano wa kikanda ikiwemo Umoja wa forodha,Soko la pamoja,Sarafu moja na Ushirikiano wa kisiasa
No comments