KAMPENI YA AWAMU YA PILI YA MATUMIZI BORA YA HABARI ZA MITANDAONI YAZINDULIWA LEO NA MAMLAKA YA MAWASILIANO (TCRA)
Mwenyekiti wa Bodi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe, (watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba, (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloga Tanzania, (TBN), Bw. Joachim Mushi, (wapili kushoto), na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Bi.Valerie Msoka, wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa awamu ya pili ya Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya mtanao yaKijamii.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akizungumza katika warsha ya siku moja na wamiliki wa mitandao ya kijamii leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu JK Nyerere
Bw. Thadeo Ringo kutoka TCRA, akiwasilisha mada iliyoelezea "Matumizi salama ya mitandao ya kijamii.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi,Bw. Mwangassa, akiwasilisha mada iliyozungumzia "Hali ya usalama mitandaoni" ambapo kwa sasa alitoa hakikisho kuwa ni salama hapa nchini.

Mwenyekiti wa TBN, Bw. Joachim Mushi, akizungumza kwenye warsha hiyo ambapo aliipongeza TCRA kwa kuwashirikisha wadau kwenye masuala ya kuelimisha kuhusu matumizi bora ya mitandao ya kijamii
Bw. Maxcence Mello, Mmiliki wa Blog ya Fikra Pevu, kwa niaba ya TBN, akiwasilisha mada iliyoelezea Maudhui ya mtandaoni na changamoto zake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Bi. Valerie Msoka, (kulia), Afisa Habari wa Mamlaka hiyo, Bi.Mabel Masasi, na Bw. Fredy Ntobi, wakijadiliana jambo
Na.Mwandishi wetu ,Dar es salaam
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA), imezindua awamu ya pili ya Kampeni ya Kusisitiza Matumizi Bora ya Mitandao ya Kijamii, uzinduzi uliokwenda sambamba na kuendesha warsha ya vyombo vya habari mtandaoni (Online Media), kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2017.
uliokwenda sambamba na warsha ya vyombo vya habari mtandaoni, (Online Media), na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam, Septemba 22, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba, alisema, TCRA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha mayumizi ya mitandao ya kijamii, yanakuwa na tija badala ya kulibomoa taifa.
“Kampeni hii inasisitiza, ukitumiwa ujumbe usiofaa, usiusambaze, ufute papo hapo.” Alisema Mhandisi Kilaba.
Alisema, TCRA inatambua uhuru wa kutoa mawazo, lakini katika kipindi hiki ambacho teknolojia ya mawasiliano inakuwa kwa kasi, ni wajibu wa chombo hicho kuwakumbusha mara kwa mara watumiaji wote wa mitandao ya kijamii, kuzingatia utamaduni wa nchi, lakini pia kuwa na uzalendo katika kutumia mitandao hiyo ili hatimaye iwe na tija kwa kila mtu.
Aidha, kabla ya uzinduzi huo, washiriki walipata fursa ya kuelimishwa mambo mbalimbali ikiwemo, matumizi salama ya mitandao ya kijamii, Maudhui ya mitandao ya kijamii iliyotolewa na Maxcence Mello kwa niaba ya TBN, na Hali ya Usalama Mitandaoni iliyowasilishwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bw. Joshua Mwangassa.
Mmiliki wa Blog ya Le Mutuz.com, Bw. William Malecela, maarufu kama Le Mutuz Nation, akizungumza kwenye warsha ya vyombo vya habari mtandaoni, (Online media), iliyotayarishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2017. Warsha hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya matumizi bora ya habari mtandaoni, (Online Media). Katika maoni yake, Le Mutuz, ameshauri TCRA, na wadau wote, kuendelea kukuna vichwa ni wapi tulikosea wakati teknolojia hii ilipoingia nchini, na hivyo kuweka mikakati ya kusimamia matumizi hayo kwani anasikitishwa na jinsi mamlaka zinavyoshughulikia malalamiko ya watu wa kawaida ikilinganishwa na jinsi mamlaka hizo zinavyoshughulikia makosa yana.yotendwa mtandaoni dhidi ya viongozi ambapo hatua huchukuliwa kwa haraka

Baadhi ya walioshiriki warsha hiyo, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wataalamu.

Katibu Mkuu wa TBN, Bw. Krantz Mwantepele

Mhandisi Kilaba, (kulia), Bi. Msoka (katikati) na Bw. Ntoni, wakiteta jambo.
.

No comments