PENZI LA MAMA STEVE LAZIDI KUMTESA BARNABAR
Mwalimu
na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic'
amefunguka na kudai anam-miss sana mama Steve 'Zuu Namela' japokuwa kwa
sasa hayupo tayari kumrudia mzazi mwenzake huyo.
Barnaba
ameeleza hayo baada ya kupita muda mrefu tokea aachane na mzazi
mwenzake huyo na kupelekea kuwa single mpaka kipindi hiki.
"Sitaweza kurudiana na mama watoto wangu japo nam-miss sana", amesema Barnaba.
Aidha,
Barnaba amesema kwa upande wake mapenzi hayajawahi kumuendesha hata
kidogo kama baadhi ya watu wengine wanavyokuwa baada ya kuachana na
wapenzi wao kwa kushindwa hata kuendelea kufanya kazi zao.
"Niwe
mkweli tu, mimi sijawahi kuendeshwa na mapenzi au mahusiano. Mapenzi
hayana nafasi kubwa katika maisha yangu japokuwa yana nguvu kwa mtu
yeyote yule, mapenzi hayajawahi kuchukua asilimia kubwa ya maisha yangu,
kuniathiri wala kunitikisa", amesema Barnaba.
Pamoja
na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Kila unachokiona kinatokea
katika maisha yako kiwe kizuri au kibaya ni mapito tu, kwa sababu
kilichotuleta duniani ni kingine na tunachokifanya ni kingine kwa hiyo
muda mwingine kutendwa na vitu vingine ni kutenda dhambi zaidi 'so
sometimes' unatakiwa upokee kwa furaha chochote utakachokumbana nacho
katika maisha yako, kwa sababu hujui mpango wa Mungu ukoje. Ninachoamini
mimi ni kwamba nilikuwa napita kwenye daraja ili niweze kuendela na
safari aliyopanga Mungu 'so' sijui 'next' nilichopangiwa na Mwenyezi
Mungu", amesisitiza Barnaba.
Kwa
upande mwingine, Barnaba japo wameachana na Zuu lakini bado
wanamawasiliano mazuri baina yao na kudai hivi karibuni aliongea naye
kuulizia maendeleo ya Steve ya kimasomo na kumtumia pesa kwa ajili ya
matumizi ya shule.

No comments