DC KILOLO AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO WAO
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akiwa katika ziara ya kuzitembelea
shule za msingi za kata ya Bomalang'ombe na kujionea jinsi gani shule
hizo zinavyoongozwa na kuzitambua changamoto zinazowakabili
walimu,wanafunzi,wanachi na viongozi wanaozizunguka shule hizo lengo
likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa wilaya ya
kilolo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bomalang'ombe.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanachi
wa kijiji cha mwatasi wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kufanya vizuri
katika masomo ya shule ya msingi kutokana na wazazi kutowatimizia
mahitaji muhimu watoto wao pindi waendepo shule.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika katika shule hiyo mwalimu mkuu wa
shule ya msingi mwatasi Seth Mfikwa alisema kuwa wazazi wengi wa kijiji
hicho wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa
juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa
kijijini wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa
watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii
mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Mfikwa
Mfikwa
alimuomba mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kutafuta wataalam wa
saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kijiji cha Mwatasi ili kukuza
taaluma kwa wanafunzi wa kijiji hicho.
“Ukiangalia
hali ya ufaulu wa shule hii sio mzuri kutokana na wazazi kutokujua
umuhimu wa elimu lakini tunaendelea kuwaelimisha kidogo kidogo hivyo kwa
kuwa mkuu leo umefika kwenye shule yetu tunaomba msaada wako wa kutoa
elimu kwa wazazi ili kukuza elimu kwa wanafunzi wa kijiji hiki” alisema
Mfikwa.
Aidha
Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini
bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa
kuwa bila hivyo watoto wa kijiji hichi wataendelea kuwa wafanyakazi za
ndani tu.
Anderson
Mdeke ni diwani wa kata ya Bomalang’ombe alikiri kuwa wazazi wa kijiji
cha mwatasi hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika
maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kweli
kabisa wazazi wa kijiji cha mwatasi wamekuwa wakiwaambia watoto
wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na
gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za
ndani na dio furaha kwa wazazi wa kijiji cha Mwatasi” alisema Mdeke
Mdeke
alisema kuwa uongozi wa kata ya bomalang’ombe utaendelea kutoa elimu
kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu
yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.
“Zana
potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa
kijiji cha Mwatasi hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi
wa kijiji hichi” alisema Mdeke
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliahidi kulifanyia
kazi tatizo hilo kwa kuzungumza na wazazi ili kuwaelimisha juu ya
umuhimu wa elimu kwa wananchi wa kijiji hiki cha Mwatasi.
“Tangu
nianza ziara katika wilaya ya kilolo leo ndio nimekutana nah ii
changamoto ya wazazi kuwarudisha nyuma kielimu hivyo nitatenga muda
muafaka wa kuja kuongea na wazazi wa kijiji cha Mwatasi kwanza swala
hili limenishtua sana kwakweli lazima nilitafutee ufumbuzi haraka
sana”alisema Abdallah
Aidha
mkuu wa wilaya hiyo Asia alisema anatakiwa kujifunza tabia za wananchi
wa kijiji cha Mwatasi kwanini wanafanya hivyo kwa kuwa changamoto hiyo
ni kubwa na inatakiwa kutatuliwa mapema.
“Unajua
lazima nijue chanzo cha kuwakatisha tamaa watoto wao wasiendelee na
masomo ni nini hivyo nikijua tatizo ni nini naweza kutatua tatizo hilo
kwa urahisi kabisa maana elimu ni kitu mhimu sana kwa maendeleo ya
watoto yao” alisema Abdallah
Abdallah
alisema licha ya changamoto hiyo ya wazazi hata walimu wa shule
wanamatatizo kwani haiwezekani kuwa na walimu wengi hivi lakini ufaulu
bado upo chini lazima kukaa chini na hawa walimu kujua tatizo ni nini.
No comments