MKURUGENZI WA MAENDELEO YA JAMII AWAONGOZA WANANCHI WA KIJIJI CHA MONDO KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA MONDO, MISUNGWI.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Sera
ya Maendeleo ya Jamii pamoja na mambo mengine, inaelekeza jamii
kushiriki kazi za kujiletea maaendeleo yao wenyewe maana jamii ndiyo
kitovu cha maendeleo.
Kwa
kutambua hilo, Mkurugenzi wa Maendelo ya Jamii Bw. Patrich Golwike
ametembelea katika Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo, kilichopo katika
Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuhamsha ari ya wananchi kushiriki
katika ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha kijiji chao.Bw.
Golwike alibainisha kuwa maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe na hakuna mtu
kutoka nje ya eneo fulani ataleta maendeleo katika eneo husika.
“Sisi
hatukuja hapa kijijini Mondo kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Kituo
cha Afya Mondo, bali tumekuja kuhamsha ari ya wananchi wa kijiji hiki
kuwa tayari kushiriki kazi za maendeleo yao kwa kutumia rasilimali
zilizopo” alisema Bw. Golwike.
Naye
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo Bi. Aziza Omary alibainisha kuwa mradi
wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo uliibuliwa kwenye kikao cha
Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mondo, ndipo iliporidhiwa kujenga kituo hicho
ili kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, na
pia kuondokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya za rufaa
zikiwemo za wazazi na wagonjwa wengine.
Awali
wananchi walishiriki kubaini changamoto, kupanga, kutekeleza na
kusimamia mradi wa ujenzi kuhakikisha kuwa wananchi wanajitolea
kuchangia nguvu kazi zao katika zoezi la ujenzi.
Kazi
nyingine zinazofanywa na wananchi ni kukusanya vifaa vya ujenzi kama
vile mawe, kokoto, mchanga, mafundi, na utoaji uchangiaji wa rasilimali
fedha.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mondo Bw. Philipo Suleiman
ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
kwa kuchagua kutembelea kijiji cha Monde mio ngoni mwa vijiji takribani
900 vilivyopo katika mkoa wa Mwanza.
Jengo
la Kituo cha Afya cha Kata ya Mondo linakadiriwa kukamilika mwaka 2018
na litagharimu takribani shilingi 150,460,540/- fedha ambayo itatoka kwa
wahisani na wananchi wenyewe.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akishiriki ujenzi wa jengo la
Kituo cha Afya katika Kijiji cha Mondo, kilichopo kata ya Mondo,
Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, mapema.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene akisalimiana na
akinamana wa Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo Wilaya ya Misungwi Mkoani
Mwanza wakati alipofika kijijini hapo kuhamsha ari ya wananchi kushiriki
kazi za maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira
yao.
Mratibu
wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina
Lipinga(kulia) aliyeshika chepeo) akishirikiana na wananchi kujenga
jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo Wilayani Misungwi mkoa wa
Mwanza kutatua kero ya ukosefu wa huduma za afya katika kata ya Mondo
kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene(kushoto
walioshika chepeo) akichanganya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, Kata ya Mondo kilichoko Wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza katika kuhamsha ari ya kushiriki kazi za
maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira husika.
Mkuu
wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi, Misungwi Mhandisi Harold J.
Mtyana akishiriki kujenga jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo,
kata ya Mondo, wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi mifuko 50 ya
simenti kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo
Bw. Marthias Lumwagila kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa Kituo
hicho cha Afya.
Sehemu
ya jengo la kituo cha Afya cha Mondo, Kata ya Mondo,Wilaya ya Misungwi
mkoani Mwanza kama linavyoonekana na wananchi wakiendelea na kazi ya
ujenzi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW.
No comments