REPSSI YATOA MAFUNZO KWA WATOTO KUTOKA NCHI 13


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Repssi chini Tanzania Edwick Manakala. Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wakiingia ukumbini tayari kwa darasa kuanza.Picha na Vero Ignatus Blog.
Muwezeshaji wa mafunzo hayo Richard Mabala akiwa anafundisha watoto pamoja na wawakilishi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania. Picha na Vero Ignatus Blog.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika wakifuatilia kwa makini yale yanayoendelea katika mafunzo hayo. Picha na Vero Igbatus Blog.
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi Boke Wambura kutoka Geita nae alihudhuria mafunzo hayo mkoani Arusha yaliyofanyika Katika hoteli ya Lushgadern. Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus, Arusha.

Shirika lisilo la Kiserikali la Reppsi limeendesha mafunzo ya siku mbili mkoani Arusha kwa watoto kutoka nchi 13  huku wakihimiza maneno makuu matatu mtoto anahitaji Upendo ulinzi anahitaji kuona wazazi wakimjali

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo yaliyomalizika leo Mkurugenzi Mkazi chini Edwick Mapalala amesema kuwa lengo kubwa la shirika hilo lililoanzishwa mwaka 2001 ni kutoa huduma ya malezi na makuzi ya watoto kwa kutilia mkazo mahitaji ya watoto ya kisaikolojia

Amesema kuwa Kutokana na maswala ya ukimwi na Maswala ya migogoro ndani ya familia imepelekea watoto wengi kuishi maisha hatarishi ambapo wazazi, walezi hawana muda wa kutosha wa kukaa na watoto Kama ilivyokuwa zamani,amesema wanatoa elimu kwa waalimu, wazazi na walezi ili kumpatia mtoto malezi anayostahili akue vizuri  na ustawi wake wa kisaikolojia uwe imara 

Ametoa wito kwa jamii nataifa kwa ujumla na kusema kuwa kama jamii inataka kuwa na watoto na vijana wenye maarifa na ustawi uliobora kila mmoja apende familia yake na atenge muda wa kukaa na familia yake.

Bi.Edwick amesema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni baadhi ya wazazi wanatilia mkazo zaidi kwenye kazi ,hawana muda wa kutosha na familia, watoto jambo ambalo limepelekea watoto wengi wanalelewa na wasaidizi,ameongeza kwa kusema kuwa kila mtoto anahitaji upendo pamoja na makuzi kutoka kwa mzazi wake.

 ''Unamkuta mzazi yupo bize kazini muda wake wa kazi ukiisha anahamishia kazi nyumbani ,tutakubaliana jamii kwa sasa kwenye malezi ya watoto kuna changamoto watoto wengi wanalelewa na wasaidizi (housegirl) ukweli usiofichika ni kwamba kila mtotoanahitaji upendo, makuzi kutoka kwa mzazi wake''alisema.

Aidha amezitaja nchi hizo Angola, Botswana, Msumbiji, Zimbabwe ,Uganda,Kenya,Swazland,Lesotho,Malawi,Namibia, Afrika ya Kusini na mwenyeji Tanzania.



No comments