Meya wa manispaa ya Lindi awataka madiwani wajiendeleze kielimu.



Na.Mwandishi wetu Lindi.


MSTAHIKI meya wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo leo amelazimika kusema kitu ambacho baadhi ya madiwani na hata wabunge wasingependa kukisikia. Baada ya kuwaambia madiwani wenzake wa halmashauri hiyo wajiendeleze kieimu badala ya kutegemea mafunzo.

Lihumbo aliyasema hayo wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo kilichoketi kwa ajili ya kupitia hesabu za mwisho (final account) za mwaka wa fedha wa 2016/2017 ulioishia tarehe 30, mwezi Juni, mwaka huu. Kikao kilichofanyika katika manispaa hiyo.

Meya Lihumbo alisema ni vigumu mafunzo ambayo hutolewa kwa madiwani kwa muda mfupi kuwajengea weledi mkubwa wakuweza kuzipitia taarifa mbambali kwa ufasaha. Badala yake watenge muda wajiendeleze kielimu.

Lihumbo ambaye katika kikao hicho kunanyakati aligeuka kuwa kama mwalimu, alisema madiwani wanapaswa kutenga muda kwaajili ya kujiendeleza badala ya kutegemea mafunzo ambayo kimsingi hayawezi kuwajengea weledi mkubwa. Hasa kuhusu taarifa za fedha.

Alisema japokuwa mafunzo yanasaidia, hata hivyo mambo mengine, ikiwemo hesabu ni vigumu kumfundisha mtu kwa muda mfupi na kumfanya awe nauwezo wa kupitia na kuchangia taarifa kwa ufanisi mkubwa.

“Nikweli waheshimiwa madiwani mliomba mafunzo, lakini mambo mengine ni vigumu kufundishwa kwa muda mfupi mkaelewa. Mambo ya mahesabu niyakitaalamu ni vigumu kuelewa kwa muda mfupi,” alisisitiza Lihumbo.

Licha ya kesi ya mahesabu na mafunzo, Lihumbo alilazimika kuingia darasani tena nakuanza kutolea ufafanuzi majibu ya maswali ya baadhi ya madiwani waliotaka kujua kwanini taarifa hiyo imeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

Kuhusu hilo alisema; “Hayo mnayoona yameandikwa kwa lugha ya kiswahili ndio hayohayo yaliyoandikwa kiingereza. Bali taarifa itakayopelekwa kwa mkaguzi ni hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza, na ndio nitakayosaini mimi. Kesho msije kushangaa kwanini nilisaini iliyoandikwa kiingereza,” aliwatahadharisha.

Awali baadhi ya madiwani wali hoji sababu za kutolewa mafunzo ambayo waliomba wapewe ili kuwajengea uwezo wa kupitia taarifa kama hizo. “Mheshimiwa mwenyekiti hawa wauza duka wetu wanapoleta taarifa za hesabu kwetu sisi wenye duka walenge kuwasiliana na sisi. Tulishasema mahesabu niyakubebana bebana tupewe mafunzo. Halafu inaandikwa kwa lugha ya kiingereza. Kwanini kiswahili kisipewe kipaumbele,” alisema mmoja wa madiwani.

Mbali na Lihumbo, mtu mwingine ambae ilibidi afanye kazi ya ziada ili aeleweke na baadhi ya madiwani ni mtunza hazina wa halmashuri hiyo, Mohamed Mkwawa. Ambae alilazimika kuwaonesha madiwani hao vifungu vilivyoandikwa kwa kiingereza nisawa na kifungu cha ngapi kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili.

Juhudi za Lihumbo na mtunza hazina zilisababisha madiwani hao kuridhia taarifa hiyo ipelekwe katika hatua nyingine kwa hatua inayofuata. Kwamujibu wa sheria, miongoni mwa sifa za msingi za wabunge na madiwani nikujua kusoma na kuandika tu.

No comments