Anusurika kipigo baada kwa kumuozesha binti wa miaka 13
Mwanamke mmoja mkazi wa kitongoji cha Natema kata ya Kiranyi Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amenusurika kipigo cha wananchi wenye hasira baada ya wananchi kutambua kwamba mwanamke huyo amemuozesha binti yake wa miaka 13 usiku saa saba wakati wakati watu wamepumzika.
Akizungumza jirani ambaye anaishi jirani na nyumba hiyo iliyotokea tukio hilo Losuye Mwivalo amesema kuwa yeye amlishuhudia vijana ambao hakutambua idadi yao wakimchukua binti huyo na kumpakia ndani ya gari na kuondoka naye ambapo wakati huo mama yake mzazi ndiye aliwapa kibali cha kumchukua mtoto huyo.
Kufuatia hayo diwani wa kata hiyo ya Kiranyi Mh John Seneu Jombi alilazimika kufika eneo hilo na kuwaomba wananchi wasimpige kwasababu ni kosa kujichukulia sheria mkononi kwasababu ni kinyume cha utaratibu na akawasihi wampeleke kituo cha polisi cha Ngaramtoni ili akahojiwe na polisi kuwa mtoto yuko wapi kwasababu mama huyo amesema hajui mtoto alipo.
Kwa upande wa mama ambaye amehusika na tukio hilo amesema kuwa yeye hajui lolote lakini mume wake ndiye aliyetoa kibali cha binti yao kuolewa akiwa mdogo kwa hiyo wananchi wanamuonea bure kwasababu yeye alitekeleza alichokuwa anaambiwa na mumewe.
Wananchi hao ambao wamekerwa na tukio hilo wamesema kuwa hawakubaliani na uamuzi wa mama huyo ambaye amemnyima mtoto huyo haki zake za msingi na kumuozesha akiwa na umri mdogo ambaye amemaliza shule hivi karibuni.
Wananchi hao ambao ambao wamesema wamemheshimu tu diwani wao lakini walikuwa wanataka wamfunze adabu kwasababu kama Raisi Magufuli anataka watoto waende shule na wanaozeshwa kinyume cha taratibu siyo jambo zuri hivyo wakamua kumpeleka mwanamke huyo kwenye kituo cha polisi cha Ngaramtoni ili aeleze ni wapi ambapo mtoto amepelekwa
No comments