Kuondolewa kwa waliovamia eneo la Ikolojia ya Tarangire na Manyara
Siku 14 zimetolewa kwa Wafugaji na wakulima waliovamia na kuweka makazi katika eneo la Ikolojia ya hifadhi ya Tarangire na Manyara, waondoke kabla ya wametakiwa kuondoka kabla kuanza operesheni ya kuwaondoa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Babati Mhandisi Raymond Mushi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja, wavaamizi hao wanaoishi ndani ya eneo hilo,wakilima na kufuga walitakiwa kuhama lakini wamekaidi.
"Tunatarajia kuanza operesheni kuwaondoa wote watakaokaidi kwani tayari wametengewa maeneo ya kuhamia na serikali za vijiji lakini wamekaidi"alisema
Amesema kuwa kuna wafugaji kaya 17 zinaishi ndani ya maeneo ya mapito ya wanyama lakini pia kuna wakulima na wavuvi haramu ambao wameanza kuweka makazi katika maeneo hayo hatua ambayo pia inachangia pia vitendo vya ujangili na ukataji wa misitu kwa ajili ya mkaa.
Kwa upande wake mtaalam wa masuala ya uhifadhi,Lucas Ole Mukusi alisema ni vyema wananchi kufuata mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuepuka hasara ya kuhamishwa katika maeneo yao.
Aidha Ole Mukusi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, amesema ili kuhakikisha hifadhi za Tarangire na Manyara zinabaki salama ni lazima kulindwa eneo la mapito ya wanyama, kwani pia kutasaidia wanyama kukuza vizazi vya wanyamapori.
"Hivi sasa hifadhi hizi zinakwenda kuwa visiwa, sasa itakuwa vigumu wanyama kuhimili magonjwa kama wakizaliana wao kwa wao bila kutoka nje ya wanyama wa maeneo mengine"alisema
Hata hivyo, alishauri operesheni za serikali kujali utu lakini pia kuhakikisha wavamizi kama ni wakazi halali wa vijiji wanapelekwa maeneo yaliyotengwa.
Mwenyekiti wa kijiji cha vilima vitatu, Erasto Belela alisema tayari wafugaji wa jamii ya kibargeig ambao wanaishi ndani ya hifadhi,wamepewa eneo la ekali 500.
"tumewatengea eneo la ekali 500 pale Mfulang'ombe ili wahamie na mifugo yao lakini wamegoma"alisema
Baadhi ya wafugaji walieleza kupinga kuhama kwani hawakushirikishwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi.
No comments