Halmashauri zashauriwa kutoa ushirikiano na maofisa ushirika.

Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Halmashauri nchini zimehimizwa na kukumbushwa kuwapa ushirikiano mkubwa maofisa wa idara za ushirika ili kurahisisha ukusanyaji na kuongeza mapato yake ya ndani.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na mrajisi wa tume ya maendeleo ya ushirika, Tito Haule alipozungumza wakati wa mkutano wa wadau wa korosho wa mkoa wa Lindi, uliofanyika Ngongo, manispaa ya Lindi.
Haule alisema ipo dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu, kuwa idara ya ushirika haiongezi mapato katika halmashauri. Hali inayosababisha kuonekana sio idara muhumu. Alisema idara ya ushirika ikitumiwa vizuri itarahisisha ukasanyaji na uongezaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hizo.
Haule alibainisha kwamba njia mzuri na yauhakika katika kuitoa jamii katika umaskini na kujenga uchumi imara ni ushirika. “Ukizungumzia SACCOS, VICOBA na vyama vya ushirika vya mazao ya kilimo ni ushirika,” alisema Haule.
Mrajisi Haule alisema kupitia uratibu na usimamizi mzuri wa maofisa wa idara ya ushirika itakuwa rahisi kukusanya mapato. Huku akiwataka maofisa wa idara hiyo kuepuka kuwasehemu ya watu wanaokwamisha dhamira njema ya serikali kuhusu ushirika kwa wananchi. “Jiupusheni na kuingiza siasa katika utendaji wenu, zingatieni na simamieni taratibu, kanuni na sheria”, alionya Haule.
Ununuzi wa korosho katika msimu wa 2017\2018 unatarajiwa kuanza tarehe Mosi, mwezi Oktoba, mwaka huu. Ambapo korosho zenye ubora wa daraja la kwanza zitauzwa na kununuliwa kwa shilingi 1450 kwa kila kilo moja.
No comments