RUVU SHOOTING YATOANA SARE NA MTIBWA SUKARI

Mchezaji wa Ruvu shooting Zuberi Dabi mwenye jezj nambari 24 mgongoni,hadi dakika 45 za kioindi cha kwanza kinamalizika Ruvu shooting walikuwa wakiongoza.Picha na Vero Ignatus Blog

Na.Vero Ignatus ,Mlandizi Pwani.

Ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo Mtibwa Sukari walikuwa mgeni wa Ruvu shooting ambapo mechi hiyo imechezwa katika uwanja wa Mabatini Mlandizi matokeo yamekuwa sare ya bao 1 kwa 1

Timu ya kwanza kuliona lango la mwenzake ilikuwa Ruvu shooting ambapo goli lilifungwa na Zuberi Dabi mwenye jezi nambari 24 mgongoni hadi dakika 45 zinamalizika Ruvu shooting walikuwa wanaongoza.
Dakika ya 45 Mtibwa Sukari waliweza kusawazisha bao hilo kwa kufugwa na Mchezaji Stamil Mbonde mwenye jezi nambari 25 mgongoni

Kwa upande wake msemaji wa Mtibwa sukari Thobius Kifaru amesema kuwa mchezo huo kwao ni ushindi mkubwa
"Ruvu shooting wapo nyumbani na walikuwa wanahita  kupata ushindi leo kwani mara baada ya kufanya vibaya katika kwa michezo 3 iliyopita ambapo
Walianza na simba,mchezo wa pili wakatoka sare na Kagera,na mchezo wa tatu wakatoka sare na Lipuli" Alisema

Aidha Thobius amejitapa kuwa wao kama mtibwa sukari wamejipanga vilivyo hawakubaliani na kushindwa watapambana hadi mwisho kuhakikisha kuwa wanapata nafasi za juu

Kwa upande wake msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kuwa matokeo waliyoyapata hayajawafurahisha kwani walitarajia  kupata pointi 3 hilo ndilo lililokuwa lengo lao kubwa

Amesema kuwa Mtibwa ni timu kubwa lakini  wamekwea kisiki kwa kukutana na Ruvu shooting

Aidha amesema kuwa mapungufu waliyoona watafanya marekebisho ili wanapikutana Jumamosi na timu ya Njombe mji waweze kuzipata point 3 wanazozihitaji.

No comments