UNICEF na TASAF KUBADILI FIKRA ZA UMASIKINI KWA VIJANA TANZANIA





 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (mwenye tai nyekundu) akiwa na uongozi wa UNICEF (Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ulrike Girbert-Nandra kulia kwake) na kushoto kwake uongozi wa TASAF.




 Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ulrike Girbert-Nandra,akifafanua kuhusu mradi wa CASH PLUS uliozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.



 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (mwenye tai nyekundu) na
Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ulrike Girbert-Nandra, wakiwa wameshika vitabu vya muongozo wa utekelezaji wa mradi wa CASH PLUS unaolenga kubadili mtazamo kwa vijana wa miaka 14-19 katika ujasiriamali na kujiwekea akiba ili kuondokana na umasikini, uzinduzi wa mradi huo umefanyika jana Jijini Mbeya.



 Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla,
Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ulrike Girbert-Nandra na viongozi wa TASAF na waalikwa waliofika katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya katika uzinduzi wa mradi wa CASH PLUS unaolenga kuwabadili mtazamo vijana wa Tanzania katika ujasiriamali na kujiwekea akiba ili kuondokana na umasikini. 



 Tunajadili jambo.....





 Baadhi ya vijana walengwa wa mradi wa CASH PLUS.



Tunasikiliza.

NA GORDON KALULUNGA, MBEYA

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) na mfuko wa utekelezaji wa kijamii (TASAF) leo wamezindua mradi wa Afya na ujasiriamali kwa vijana unaowalenga vijana wa kike na kiume wenye umri wa miaka 14-19 na kujulikana kwa jina la CASH PLUS.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya, Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ulrike Girbert-Nandra, alisema kuwa mradi huo unalenga zaidi vijana hao kutoka katika kaya masikini ili kuhakikisha wanakua vizuri kuelekea utu uzima wakiwa na afya na uwezo wa kuzalisha mali Tanzania.

“Kwa ushirikiano huu mwema wa UNICEF, TASAF na Wizara ya Afya, jinsia, maendeleo ya jamii jinsia na watoto, mradi huu utatoa msaada wa ziada wa kuwabadili kimtazamo vijana kuhusu umasikini na kufikia lengo la kuwa vijana wenye tija katika taifa na jami” alisema Ulrike.

Akizindua mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, aliwashukuru UNICEF na TASAF kwa kubuni mradi huo ambao unatekelezwa katika wilaya mbili za Rungwe mkoani Mbeya na Mufindi mkoani Iringa.

“Ni bahati iliyoje mradi huu kuanzia katika wilaya hizi maana kuna Halmashauri nyingi nchini hivyo serikali itasimamia vema na kuhakikisha vijana wanajifunza vema kuwa na mtazamo chanya wa kufanya biashara na kujiwekea akiba ya fedha wanazozipata” alisema Makalla.

Aliwasihi vijana ambao watanufaika na mradi huo kuwa wajiepushe na kupata gonjwa la Ukimwi bali wawe kielelezo cha jamii na kuwa wakufunzi wema kwa wenzao ambao hawajabahatika kuwemo katika mradi huo wa CASH PLUS.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Taifa, Fariji Misha alisema mpango huo utaleta manufaa makubwa kwa walengwa na kujenga nguvu kazi

“Siyo watoto wote wanaochaguliwa kuendelea na masomo hasa wanaohitimu elimu ya msingi na sekondari hivyo wakiachwa hivi hivi mtaani hasa wanaotoka katika kaya masikini wanaweza kuingia katika mambo ambayo si kwamba yanaweza kuharibu tu maisha yao, bali yanalinyima taifa nguvu kazi yenye ufahamu bora” alisema Misha.

Alisema taifa lenye kuishia kuwa na vibarua haliwezi kufanya maamuzi ya msingi, hivyo kupitia CASH PLUS, vijana hao watapewa mafunzo ya stadi za maisha katika mpango wa kuweka akiba na kuwekeza pamoja na elimu ya afya ya uzazi na UKIMWI, hivyo Halmashauri tekelezeni mpango huu kwa ufanisi unaotakiwa.

Kwa upande wao baadhi ya vijana wanufaika wa mradi huo Baraka Mwamakula kutoka Halmashauri ya wilaya ya Rungwe na Ruth Mussa kutoka Halmashauri ya Mufindi walisema kuwa mradi huo utawawezesha kubadili mtazamo wa kuchagua kazi za kufanya na kujifunza zaidi kuweka akiba

No comments