Basi La Tashriff Lateketea kwa Moto Tanga

Basi la Abiria kutoka kampuni ya Tashriff lililokuwa linatokea Tanga kuelekea Dar limetekete kwa moto

Na .Mwandishi wetu Tanga

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kwamba ajali hiyo imetokea saa nane jana machana katika eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.

Aidha Kamanda Wakulyamba amesema basi hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Hemed Ali (35) lilikuwa na abiria 29 ambapo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.

"Hakuna aliyejeuhiwa wala kupoteza maisha imeteketea kwa moto"alisema

Wakulyamba na kusisitiza kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo cha moto huo

Mashuhuda wa  tukio hilo wamesema wameona moshi ukitoka chini ya basi hilo ndipo wakapiga kelele na kusababisha dereva kusimama dakika chache baada ya hapo likaanza kuwaka moto.

"Tumesikia kelele kutoka kwa watu waliokuwa nje tukaona dereva kasimamisha basi muda si mrefu moshi ulianza kutoka mara moto ukalipuka"amesema Bahati Mussa abiria wa basi hilo.



No comments