DKT MWAKYEMBE AFUNGUA TAMASHA LA 36 LA TASUBA


Waziri wa habarib,utamaduni ,sanaa na michezo Dkt.Harryson Mwakyembe (katikati) wakikata keki kuashiria kuwa Tamasha la 36 la kimataifa la maonyesho ya utamaduni na sanaa kufunguliwa rasmi.Picha na Vero Ignatus Blog

Baadhi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nchi tofauti walioshiriki katika Tamasha hilo la maonyesho ya sanaa na utamaduni linaloendelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Waziri Dkt.Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Bagamoyo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Wadhamini wa Tamasha hilo wakiwa katika picha ya pamoja na waziri Dkt.Mwakyembe ambae ndiye alikuwa mgeni rasmi .Picha na Vero Ignatus Blog


Wakazi wa Bagamoyo pamoja na wageni mbalimbali kutoka nje ya wilaya hiyo waliojitokeza katika Tamasha hilo.picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus ,Bagamoyo.

Waziri wa habari ,utamaduni,sanaa na michezo Dkt.Harryson Mwakyembe amefungua rasmi maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Maonyesho ya sanaa na Utamaduni(TASUBA) Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani

Kauli mbiu katika maonyesho hayo ya siku saba ni sanaa  utamaduni katika piga vita madawa ya kulevya,ambapo tamasha hili linalenga kulea,kueneza na kuutunza  utamaduni wa Tanzania,tamasha hili limeleta mwamko mkubwa nadani na nje ya nchi.

Mwakyembe amesema kuwa tamasha hilo tangia kuanzishwa kwake limeleta mwamko mkubwa ndani na nje ya nchi ambapo amesisitiza kuwa utamaduni na sanaa siyo la maonyesho ya jukwaani tu bali  kuna ufundi,warsha mbalimbali,kiungo cha kujenga mahusiano mazuri na wasanii mahiri wa ndani na nje ya nchi ili kuonyesha utajiri wao walionao katika sanaa

Tamasha hilo limeshirikisha mataifa mbalimbali iikiwemo Kenya,Ufaransa,Uingereza,Zimbabwe na nchi nyingine likiwa na malengo mahususi katika kuunga mkono kupiga vita dhidi ya usafirishaji na utumiaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.

No comments