WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WATOTO WAO
Ofisa
Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai (kushoto), akitoa mada katika
kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi lililofanyika
Makao Makuu ya TGNP Mabibo Dar es Salaam jana. Kongamano hilo
liliandaliwa na TGNP.
Mwanafunzi Leila Kisinga kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanamke vinavyofanya kazi.
Kongamano likiendelea.
Mshiriki Idd Hamisi akichangia jambo katika kongamano hilo.
Usikivu katika kongamano hilo.
Aisha Kijavara akichangia.
Wakina mama wakiwa katika kongamano hilo. Wakina mama hao walitoa uzoefu wao kuhusu afya ya uzazi kwa watoto.
Mwanafunzi Juma Nasoro kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanaume vinavyofanya kazi.
Mdau Selemani Bishagazi akichangia kuhusu wanaume kuwasaidia watoto wao wa kike wanapokuwa katika hedhi.
Mary Mbarawa akichangia jambo.
Na Dotto Mwaibale
WAKINA
Baba nchini wametakiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao
badala ya kuwaachia kazi hiyo ifanywe na wakina mama pekee.
Mwito
huo umetolewa na Selemani Bishagazi wakati akichangia mada katika
kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi kwa watoto hasa
wa kike lililoandaliwa na TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam jana.
"Suala
la utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wetu hasa wa kike ni
letu sote kati ya baba na mama kwani baba ndie chanzo kikubwa cha mapato
katika familia" alisema Bishagazi.
Bishagazi
alisema suala la kutoa fedha za kunulia pedi wakati mtoto wa kike
anapokuwa kwenye hedhi si la mama bali hata baba anawajibu wa kutoa
fedha hizo na akaomba dhana hiyo potofu kuwa mama ndiye anawajibika
katika suala hilo iachwe.
Alisema
ni vizuri mtoto wa kike anapokuwa katika hedhi kuwajulisha wazazi wake
ili aweze kusaidiwa kupata fedha za kununulia pedi badala ya kukaa kimya
kwa hofu na kujikuta akishindwa kujistiri na kuchafuka.
Mshiriki
mwingine katika kongamano hilo alisema usiri imekuwa ni changamoto
kubwa katika kumsaidia mtoto kujua afya za uzazi kwani wazazi wengi
wanashindwa kuwaweka wazi watoto wao kuhusu jambo hilo.
Alisema
mtoto wa kike anapobalee na kuanza kuingia katika hedhi wazazi
wanapaswa kumueleza kuwa amekuwa na hivyo iwapo atakutana na mwanaume
atapata mimba hivyo kumpa elimu hiyo kwa wazi ataweza kujiepusha na
kupata mimba badala ya kufanya siri.
Aisha
Kijavara ambaye alishiriki katika kongamano hilo alisema ni vizuri
elimu ya afya ya uzazi ikatolewa kwa uwazi na kutaja viungo vya uzazi
bila ya kuona aibu ili watoto waweze kuelewa vizuri badala ya
kufichaficha.
"Katika
suala ili la utoaji wa elimu hii ya afya ya uzazi tunapaswa kuwa na
muda wa kutosha na kutamka wazi viungo vya uzazi jinsi vinavyofanya kazi
ili walengwa waweze kuelewa vizuri somo" alisema Kijavara.
Ofisa
Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai alisema wanapopigania bajeti
zinazopitishwa na bunge ziwe na mlengo wa kutoa kipaumbele kijinsia
zinamlenga zaidi mtoto wa kike ambao wanachangamoto nyingi hasa wale
waliopo mashuleni kwani wengi wao hawana uwezo wa kununua pedi
wanapokuwa katika hedhi.
Alisema
baadhi yao wamejikuta wakiingia katika vishawishi vya kuwa na uhusiano
wa kimapenzi na wanaume ambao wamekuwa wakiwasaidia kuwanunulia bedi.
"Tumekuwa
tukihimiza kutengwa kwa bajeti kubwa za wizara husika ili kuwasaidia
watoto hawa ambao wapo katika changamoto hiyo" alisema Sangai.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa na Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Mabibo
ambao baadhi yao walitoa mada kuhusu afya ya uzazi na matumizi ya via
vya uzazi.
No comments