RAIS MAGUFULI AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KABLA YA MWISHO WA MWEZI HUU WAWE TAYARI WAMENUNUA DAWA ZA VIUAWADUDU WA MALARIA
Na.Vero Ignatus Kibaha,Pwani
Rais Dkt.Magufuli amefanya ziara katika kiwanda cha
kutengeneza dawa za kuulia vimelea vya mbu wanaosababisha malaria
kilichopo Kibaha, Pwani.
Katika ziara katika kiwanda hicho ametoa siku 10 kwa Halmashauri zote nchini kwenda kuchukua dawa za kuua wadudu wa malaria wanaokuwa kwenye maji yaliyotuama na kupulizia katika maeneo ya makazi ya watu
"Nataka tatizo la watanzania kuugua malaria liishe kabisha nataka nione wagonjwa wamepungua hospitalini ,na nyie wenye kiwanda tengenezeni madawa yenye kiwango,naomba kiwanda kifanyae kazi na wafanyakazi walipwe mishahara yao."alisema Magufuli
Awali,
Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Samweli Mziray alimweleza Rais kuwa dawa
takribani lita 100,000 zipo tu kiwandani hapo baada ya wanunuzi wakuuu
ambao ni Halmashauri za Wilaya kushindwa kuzinunua kwa madai ya kukosa
fedha ambapo lita moja ya dawa hiyo inauza shilingi 13,200
Kadhalika,
Rais ameiagiza Wizara ya Fedha kutoa Sh1.3 bilioni kwa ajili ya
kulipia dawa hizo za kuua vimelea vya mbu zilizopo katika
kiwanda ambapo ametoa wiki moja fedha hizo ziwe zimeshawasilishwa kiwandani hapo.
“Sasa
mimi nimeshatoa agizo dawa zilipiwe, sasa nione mkurugenzi ambaye
atashindwa kutekeleza agizo langu la kufata dawa hizo kwa kipindi
nilichotoa, nimesema natoa muda mpaka mwisho wa mwezi, "amesema Rais
Magufuli.
Rais amesema kuwa Watanzania wapo tayari kwenda kununua madawa nje ya nchi kwa gharama kubwa wakati hapa nchini kuna kiwanda kipo na kinatengeneza dawa ya kuua viluilui vya malaria.
"Kiwanda kimekuwa tayari watanzania hawataki kununua dawa."alisema

No comments