MZEE YUSUPH ATAJA SABABU ILIYOMFANYA AACHANE NA MUZIKI
Aliyekuwa
mwimbaji wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ambaye kwa sasa anafahamika
kama Alhaj Mzee Yusuph amefunguka kuhusu kuacha kwake muziki na kufanya
toba ili kurudi kuwa muumini na kutoa daa’wa.
Akizungumza kwenye Leo Tena ya Clouds FM Alhaj Mzee Yusuph amegusia pia
jinsi maneno ya watu yalivyofuata baada ya kutangaza na hatimaye kuacha
kabisa muziki huku akielezea namna alivyokuwa anakataza watu kwenye
Kundi lake wasitende maovu.“Mimi
nimeacha muziki kwa sababu nataka kuwa Muumuni wa Dini ya Kiislamu na
kumfuata Mtume Muhammad (SAW). Nilipopata nafasi ya kwenda kuhiji Makka
na kushika Al Kaaba nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu.
“Nilipoanza
kubadilika nilikuwa nakataza pombe kwenye Band yangu. Siku nisiyowepo
walikuwa wanasema Simba leo hayupo. Nilipokuwa nakataza haya mambo wengi
walikuwa wakiniambia kwa nini nisifungue Madrasa. Kubadilika kwangu
niliachana kwanza na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa
maji tu unaposikia kiu.
“Nilizungumza
mimi na Mungu wangu nikisema: ‘Wewe ndiye mwenye kutoa msamaha’.
Nikafanya show ya mwisho Dodoma nikaachana na muziki. Nilimwambia kwanza
mke wangu mdogo mimi nimeacha muziki. Kesho yake nikamuambia mke wangu
mkubwa nimeachana na mziki, hawakuamini.” – Alhaj Mzee Yusuph.

No comments