OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAHIMIZA USHIRIKIANO NA WADAU
Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu akitoa maelezo wakati wa
Mkutano wa Kazi kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau (
hawapo pichani)kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo Mkoani
Tabora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Madhumuni ya Kikao kazi hicho ilikuwa ni kukutana wa wadau hao kwa lengo
la kujadiliana, kubadilishana mawazo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto
mbalimbali ambazo wadau hao pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wanakumbana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wadau walioshiriki kikao hicho ni kutoka Mahakama, Takukuru, Magereza,
Polisi, Wakala wa Barabara, Maliasili, Halmashauri, Mawakili wa
Serikali, Wanasheria na wanajamii. Kushoto kwa Naibu Mwanasheria Mkuu
Wakili Mfawidhierikali Kanda ya Tabora Bw. Jackson Bulashi na kulia ni
Kamanda wa Takukuru Tabora Bw. Fidelis Kalungura.
Sehemu
ya wadau ambao wamekuwa na mazungumzo na majadiliano na Ujumbe wa Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ulioongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu
wa Serikali. Bw. Gerson Mdemu. Majadiliano hayo yamefanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Takukuru Mkoani Tabora siku ya Ijumaa ( June 16)
ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Wadau
kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Mahakama, Polisi, Takukuru,
Maliasili, Magereza, Halmashauri, Wakala wa Barabara,Mawakili wa
Serikali na Wanasheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kumalizika kwa kikao kazi cha majadiliano baina ya wadau hao na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo wameazimia kuzifanyia kazi
changamoto mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho na kisha kupeana
mrejesho.
Na Maura Mwingira, Tabora
Katika
kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali leo ( Juni 16) imekutana na wadau mbalimbali mkoani Tabora kwa
madhumuni ya kujadiliana na kubadilishana mawazo yenye lengo la
kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za kiutendaji.
Akitoa
maelezo ya awali mbele ya wadau hao kutoka taasisi za serikali
zinazofanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Mdemu pamoja na mambo
mengine amesisitiza haja na umuhimu kwa wadau hao pamoja na Ofisi yake
kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ili kuiwezesha serikali
kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu.
“
Nyinyi ni wadau wetu muhimu sana sana, ni kwa sababu hiyo, katika wiki
hii ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma tukaamua kuja Mkoani Tabora ili
tukutane nanyi.
Ni
tumie basi, kikao hiki cha kazi kusisitiza kwenu, haja na umuhimu wa
kufanya kazi kwa ushirikiano na ukaribu ili kwa pamoja tuisaidie na
kuiwezesha Serikali itekeleze majukumu yake kwa ukamilifu”. Akasema
Naibu Mwanasheria Mkuu.
Akaongeza
kwamba, ni kwa kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu licha ya kwamba
kutaisaidia serikali lakini kubwa zaidi kutapuguza lawama na kunyosheana
vidole.
“ Ni
vema tutambue kuwa hakuna Taasisi ambayo inaweza kutekeleza majukumu
yake pasipo kushirikiana na Taasisi nyingine. Lakini hili halilengi au
haina maana ya kuingilia majukumu ya Taasisi au Mihimili mingine bali ni
katika kutekeleza misingi na maadili ya utumishi wa umma” akabainisha
Bw. Mdemu.
Wadau
waliohudhuria majadiliano hayo ni kutoka Jeshi la Polisi, Mahakama,
Magereza, Takukuru, Halmashauri, Wakala wa Barabara, na Idara ya Misitu
na jamii. Akifafanua ziaidi hoja hiyo ya ushirikiano. Naibu Mwanasheria
Mkuu ambaye ameambata na Wakurugenzi kutoka Divisheni zinazounda Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu. Pia amewataka wadau hao kuelezea kwa uwazi ni
ushauri wa aina gani na katika eneo gani ambao wanauomba kutoka Ofisi ya
Mwanasheria mkuu.
“Pale
mnapoleta mikataba yenu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa ushauri au
maoni, ni muhimu sana mkaweka wazi katika barua zenu ni maeneo gani gani
ya mkataba mnayotaka ushauri au maoni, na kwa sababu gani. Badala ya
kuleta maelezo ya mstari mmoja kwamba mnataka ushauri”.
Kasisitiza
“ Jukumu letu kuu na la msingi na ambalo limeainishwa katika Katiba ni
kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali na wadau wengine. Lakini ili
ushauri huo uweze kutolewa kwa ukamili,utaalamu na kwa mujibu wa sheria
inayosimamia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu . Hivyo ni lazima basi wadau wetu
wawe tayari kutoa ushirikiano kwa kuweka wazi maeneo wanayotaka
kushauriwa. Tukifanya hivi tutakuwa tunaisaidia sana Serikali”.
Wakati
huo huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewashukuru wadau hao kwa kutenga
muda wao na kuitikia wito wa kukutana na kubadilishana na mawazo ikiwa
ni pamoja na kubadilishana uzoefu.
Kwa
upande wao wadau hao wameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwa kuamua safari hii kukutana na wadau wa Mkoa wa Tabora na kwamba
mikutano ya aina hiyo ni muhimu sana katika uboreshaji wa uhusiano,
ushirikiano na utetekelezaji wa majukumu ya kila taasisi.
Wadau
hao pamoja na kutoka maoni yao na michango yao pia wameipongeza Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitekeleza
majukumu yake ya utoaji wa ushauri kwa wakati.
Katika maadhimisho ya mwaka jana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilikutana na wadau wa Mkoa wa Dar Es Salaam.
No comments