Lowassa aachiwa kwa dhamana.....Atakiwa Kuripoti Tena Alhamisi
Waziri
Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa
kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
(DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza
baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema
Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa
6.00 mchana.
Kibatala
amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya
onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa
Ukonga, Mwita Waitara.
"Mzee
amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23,
mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa
ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29," amesema.

No comments