DKT MAGUFULI: HAKUNA ATAKAYEPEWA MIMBA NA KURUHUSIWA KURUDI SHULE KATIKA UTAWALA WANGU.
Na.Vero Ignatus .Bagamoyo Pwani.
Rais Dkt.John Magufuli amepiga marufuku katika utawala mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.
Ameyazungumza hayo wakati wa kumalizia ziara yake ya siku tatu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa amekwenda kuzindua barabara ya Bagamoyo msata yenye kilometa 64 ambapo imegarimu shilingi bilioni 182.
Amesema kuwa waliozaa wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kwenye vyuo vya Ufundi stadi (VETA) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.
“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili
lakini sekondari, darasa la kwanza kupeleka walio na watoto, tunapoteza
maadili yetu, watazaa mno.
Amesema wale wote wanaohusika kuwapa mimba wanafunzi wajiandae miaka 30 itakuwa inawahusu gerezanikwani wanafanya jambo hilo kwa kukusudia.
''Na wakipelekwa huko gerezani wafanyishwe kazi ngumu ambazo akitoka huko nguvu zitakuwa zimemuishia na atajikuta amebakia na huyo mtoto mmoja".alisema.
“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.
“Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema.

No comments