WADAIWA KODI YA MAJENGO KURURUZWA MAHAKAMANI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo katika kikao kazi cha
kuhamasisha ulipaji wa Kodi ya Majengo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa
Arusha Ndg. Apili Mbarouk
akizungumza katika kikao na wanahabari cha kuwakumbusha wananchi kuhusu ulipaji
wa Kodi ya Majengo.
Baadhi ya wataalam waliohudhuria katika
Kikao cha Mkuu wa Mkoa kuhamasisha uhamasishaji wa Kodi ya Majengo.
ARUSHA
Wadaiwa sugu wa Kodi ya
Majengo katika Jiji la Arusha watafikishwa Mahakamani mwanzoni mwa mwezi Julai
endapo wataendelea kukaidi kutolipa Kodi hiyo katika kipindi hiki cha mwisho wa
mwaka wa Fedha 2016/2017 unaomalizika Juni 30.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka
Gambo katika kikao chake na waandishi wa habari kuwukumbusha wananchi kuhusu
umuhimu wa kulipa kodi hiyo mapema kabla ya hatua kazi hazijachukuliwa wale
ambao hawajalipa.
Alisema wamiliki wote
wa majengo wanatakiwa kulipa Kodi hiyo kwa mujibu wa Sheria lakini hali
hairidhishi kwani wengi wao hawajajitokeza kulipa wakati Serikali inategemea
Fedha hizo kwa ajili ya Kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Aliongeza kuwa muda
uliowekwa kwa ajili ya malipo hayo unaelekea ukikongoni: Juni 30 itakua ni mwisho na baada ya hapo
Sheria kali za Kisheria zitaanza kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kuiibia
Serikali kwa kutolipa mapato ya majengo wanayoyamiliki.
“Haiwezekani unamiliki
nyumba halafu hutaki kuchangia kodi, ninatoa rai kwa wote kulipa kwa hiari kwa
sababu baada ya hapo ni Faini ambayo ni mara tano ya kiasi kile ambacho
ungetakiwa kulipa kwa sasa au kupelekwa Mahakami kwa mujibu wa Sheria.
Naye Meneja wa Mamlaka
ya Mapato Mkoa wa Arusha Ndg. Apili
Mbarouk amesema mpaka Mwishoni wa Mwezi Mei walikuwa wameshafanikiwa
kukusanya kiasi cha Tsh Bil.1 na kwa
siku zilizobakia wanatarajia kukusanya zaidi ya kiwango walichokusanya kwa
sasa.
Pia aliongeza kuwa
katika maeneo yote ambayo hayajapimwa na kufanyiwa uthamini wamiliki watalipa
Tsh 15,000 kwa mwaka na kwa yale maeneo ambayo yamefanyiwa uthamini wamiliki
watalipa kwa kadiri ya thamani ya Majengo yao.
Aidha aliwataka
wafanyabiashara na wananchi wote kutoa na kudai risiti kwa kila biashara
inayofanyika ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanakuwa salama na hayapotei
kwa namna yeyote ile.
Katika hili tutaanza
ukaguzi katika maeneo yote ya Mji huu kuanzia kwa wafanyabiashara kuhakikisha
wanatoa stakabadhi kwa wateja wao na ambaye atabainika hajatoa atapigwa faini
ta Tsh Mil 3 na kwa mwananchi ambaye atakuwa amenunua bidhaa bila kudai
stakabadhi atatozwa faini ya Tsh 30,000.
Kikao hiki ni
muendelezo ya vikao maalumu vya Kazi anavyovifanya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
pamoja na Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Areusha kuhakikisha mapato ya Serikali
yanakusanya kwa ufanisi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Mwisho.



No comments