Katibu
Tawala wa Mkoa, Richard Kwitega amekabidhi zawadi za Eid Al Fitr kwa
mahabusu ya watoto kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Amesema "Mheshimiwa
Rais ametoa zawadi ya Mbuzi dume, mchele kilo 25 na mafuta ya kupikia
lita 10. Vitu hivyo vitawasaidia watoto hao katika kusherekea sikukuu
hiyo."
Aidha,amewapa
salamu za Rais kwa kuwataka wajue mahali pale ni pa muda mfupi tu hivyo
wakitoka wanatakiwa wakawe raia wema na wakujituma zaidi katika kazi na
wale ambao ni wanafunzi wakakazane zaidi na shule.
Wakitoa
shukrani zao watoto hao wamemshukuru sana katibu tawala kwa niaba ya
Rais, na wamempongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika kujenga taifa
hili na wao wameaidi wakitoka hapo watakuwa raia wema.
Watoto
hao wameiomba serikali kuwasaidia katika usikilizwaji wa kesi zao
zisichukue mda mrefu sana na hivyo kupelekea wengi wao kukosa masomo yao
ya shule.
Mkurugenzi
wa kituo hicho Musa Mapua, amesema tokea mwaka huu uanze ni watoto 48
wameshapita katika kituo hicho na kwa sasa wapo watoto 11 tu na wote ni
wa kiume.
Amesema
changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kituoni hapo ni ukosefu wa gari
la kubeba watoto hao pale wanapoitajika kupelekwa mahakamani na ukosefu
wa uzio kwa usalama wa watoto hao.
Hivyo ameiomba serikali kukisaidia kituo hicho ili watoto hao wawe katika hali ya usalama zaidi.
Kila
mwaka Mheshimiwa Rais amekuwa akitoa zawadi mbalimbali za Eid katika
maeneo mengi ya nchi kwa lengo la kushiriki na walengwa katika
kusherekea sikukuu.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega wa pili toka kushoto
akimkabidhi msimamizi wa kituo hicho Bw. Musa Mapua zawadi ya
Mbuzi,mchele na mafuta.
No comments