RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAHA MKOA WA PWANI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha
Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani katika siku ya kwanza ya
ziara yake ya siku tatu
Mkoani humo.
![]() |
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani. |

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwananchi Azilongwa Buhali alipokuwa akimuelezea shida yake mara baada ya kuhutubia wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
Na.Vero Ignatus Kibaha Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .John Magufuli
ameanza ziara ya siku tatu leo mkoani Pwani ambapo itajumuisha uzinduzi wa
viwanda mbalimbali mkoni hapo ,ambapo miradi mingine ya maendeleo ikiwemo barabara
itazinduliwa.
Akizungumza katika uwanja wa Bwawani Kibaha Rais ameupongeza
uongozi wa mkoa huo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuanzisha viwanda
vipya 89 ambapo katika mkoa huo vipo viwanda takribani 300 isipokuwa wilaya za Rufiji na Kibiti na hii ni kutokana
na mauaji yaliyopo ambapo amesema kwa sasa ndiyo hitimisho.
“Wawekezaji hawawezi kwenda kuwekeza katika wilaya hizo
kutokana na mauaji yaliyopo,serikali ya awamu ya tano siyo ya mchezo mchezo
watu wenye tabia hizo waache,kwani watanyooka,nawaomba msiwaunge mkono watu hao
kwani wanarudisha maendeleo nyuma ,hakuna Imani yeyote ile ya dini inayoisema
watu wauane,tuwaombee watu hao waokoke wabadilike.alisema Magufuli.
Amesema kuwa viwanda hivyo ambavyo baadhi vimeanza
uzalishaji vitatoa ajira kwa vijana na watanzania kwa ujumla ,amesema Tanzania
siyo nchi ya kuwa maskini hata kidogo kwani ni ya pili kwa kuwa na vivutio ,ina
madini ya kila aina ,25% ya nchi hifadhi na ni 3 kwa kuwa na mifugo mingi barani
Afrika
‘’Nitapambana huku nikimtanguliza Mungu,ili maisha ya
Watanzania yaweze kuendeklea mbele,hatukutakiwa kuwa maskini hata kidogo,lazima
watu wajiulize tunamahali gani tumekosea je? Na hayo makosa tuyafanyie nini “alihoji
Rais.
Amewataka viongozi wote wa serikali kujitathimini kila mmoja
kwa nafasi yake ,huku kila mmoja akijiuliza amewafanyia wananchi wa maisha ya chini
kitu gani,amesema kuwa kiongozi akishindwa kujitathimini,ndani ya miezi sita
asisubirie miaka miwili ila ajiondoe mwenyewe katika nafasi hiyo.
Aidha Magufuli amesema kuwa kila mwezi serikali inatenga
fungu bilioni 18.77 kwaajili ya kupeleka kwenye mashule sambamba na hayo
serikali imeboresha shule kwa kupeleka vyombo
1700 vya mahabara.





No comments