MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAANZA AINA MPYA YA UTALII
Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro nchini imeanza aina mpya ya utalii inayolenga
kuboresha utalii unaojali mazingira ili kuvutia zaidi watalii.
Mhifadhi
Mkuu wa mamlaka hiyo Freddy Manongi amesema, aina hiyo mpya ya utalii
inalenga kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea eneo hilo la utalii
linalotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO), lililoko kilomita 180 kutoka mji wa Arusha nchini
Tanzania.
Amesema mamlaka hiyo imeshatambua maeneo ya utalii
unaozingatia mazingira ikiwemo milima, maeneo ya kijiografia, na maeneo
ya kale, ambayo yalianzishwa miaka 58 iliyopita.
No comments