RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO;AMTAKA MKURUGENZI MKUU WA DAWASCO MUTALEMWA KUJIUZULU HARAKA KABLA MABAYA HAYAJAMPATA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini
Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na
Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani
Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kuzindua rasmi
Mradi wa huo wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi
Mkaoni Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu
Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian
Luhemeja akitoa maelezo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga
ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada
uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya
Pwani na Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga
kabla ya kudua Mradi huo wa maji.
Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo
kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani
Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu
Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS
kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya
kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi
mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ta TRL kusafirisha nondo
kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi
mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS
kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani.
PICHA NA IKULU
Na. Vero Ignatus ,Mlandizi Pwani.
Rais Dkt John Magufuli ameendelea na ziara yake mkoani pwani ambapo leo amezindua rasmi mradi wa maji wa Ruvu juu uliopo mlandizi,ambapo amezindua viwanda vitatu mkoani hapa
Akiwa Kibaha -Mlandizi Rais amemtaka Mkurugenzi wa Dawasa Injinia Ernchard Mutalemwa kujiuzulu haraka kabla mambo mabaya hayajampata
''Ninaifahamu historia yako,jiuzulu uwaachie vijana tukimbizane nao ,jina la Mutalemwa nimeanza kulisikia muda mrefu haijalishi hata kama waziri ni rafiki yako au baadhi ya mawaziri ni marafiki zako wewe jiuzulu."alisema
Katika uzinduzi huo amesema amefurahishwa sana na Dawasa na Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya japokuwa kuna changamoto nyingi wanazozipitia.
"Sasa ile dhambi ya wizara ya maji walau sasa inaanza kupungua ,ila mtu asipolipa bili hata kama ni mimi pale Ikulu wewe kata tumezowea kudekezana sana ,pamoja na nyie madeni mnayodaiwa lipeni."alisisitiza
Aidha amemtaka Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kwenda kumalizia mradi wa maji uliopo Lindi.
"mkimaliza tu Bunge hamieni huko wewe pamoja na wataalamu wako wote hadi mtakapoumaliza''alisema
Viwanda vilivyozinduliwa ni pamoja na kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi
mkoani Pwani,kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS
kilichopo Kibaha mkoani Pwani.kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS
kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

















No comments