Lowassa Amsifia Rais Magufuli Kuhusu Hatua Anazochukua Dhidi ya Madini Yetu
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kuhusu madini ya nchi yetu.
Lowassa
aliyayasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu sakata la mchanga wa madini (makinikia) ambalo limeonyesha kuwa
Tanzania impoteza zaidi ya trilioni 100 tangu mwaka 1998 hadi Machi
mwaka 2017.
“Nimpongeze
sana Mhe Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi na hatua ambazo amechukua
kuhusu jambo hili, na hasa pale anapowashirikisha wananchi, ni jambo
muhimu sana." Alisema Lowassa
Lowassa
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alisema anampongeza Rais
Magufuli kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA kwani kipindi
anazunguka kuomba kura kwa wananchi alipopita maeneo yenye madini
aliyazungumza haya yanayotekelezwa leo.
“Nampongeza
kwa kutekeleza yale maamuzi ambayo ni ya UKAWA. Nilipokuwa kwenye
kampeni ya kuomba kura, hata pale Geita, nilieleza jambo hilo, nikasema
hivyo hivyo alivyosema yeye kwamba nikiingia madarakani nitaunda tume ya
kuchunguza jambo hili ili mtanzania awe ndiye anapata sehemu kubwa ya
faida kuliko mgeni.”
Aidha,
Lowassa amesema kuwa, ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na hata
yeye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa na
kuzungumza, lakini jambo gumu lilikuwa ni kwamba, mikataba ukishaiweka
saini inakuwa migumu sana kubadilisha.
Lowassa alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo mirahaba lakini haikutosha.
“Matumaini yangu ‘figure’ (namba) hizo ni za kweli, kama ni za kweli, tumeliwa kweli kweli,” alisema
Lowassa alipokuwa akizungumzia mahesabu yaliyowasilishwa katika ripoti
za uchunguzi kuhusu kiasi cha fedha ambazo Tanzania imepoteza.

No comments