VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA NCHI WAMETAKIWA KUACHA UBINAFSI ULIOKITHIRI ,WASIWE WASANII NA WASIMDANGANYE MUNGU

Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Tanzania (KKKT)Dkt. Fredrick Shoo akiwa katika ibada katika usharika wa Kiborloni uliopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Tanzania (KKKT)Fredrick Onael Shoo
amewataka viongozi ambao wanadhamana ya kuongoza nchi waondokane na ubinafsi uliokithiri kwa
kuwadidimiza wengine ,wasiwe waigizaji ,waepuke kuwa mateka wa kupokea rushwa kwani wanaweza kuwadanganya wanadamu ila hawawezi kumficha Mugu.
Ameyasema hayo hivi karibuni mkoani Kilimanjaro katika ibada ya kumuaga aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi mjini marehemu Dkt. Philemon Ndesamburo ambapo alisema Mungu amewapa nafasi hivyo waitumie vyema kwa kutumikia nafasi zao waachane na maneno yasiyokuwa na faida.
“Wacheni
maneno maneno watendeeni wananchi mema,Mungu akikupa nafasi itumie vyema,viongozi msichoke kutenda mema fahamuni kuwa uongozi ni dhamana mtakwenda kuulizwa mlifanyaje siku ya mwisho”.alisema askofu huyo.
Aidha amesema kuwa maisha ya kila mwanadamu yana mpaka
ambao hauwezi kuuvuka kamwe kwani ikifika wakati wa kuondoka utaondoka tu hakuna kipingamizi ila
ni vyema kila mtu akaandaa maisha yake
kwani ni siri kubwa aliyoiweka kwa mwanadamu.
Askofu Dkt Fredrick Shoo aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, kusimamia katika kutenda haki na kusaidia makundi ya kijamii, kwani wapo wanaoumizwa kwa kukosa haki zao kutokana na umasikini pia aliwataka waumini na Watanzania kujifunza na kusimamia katika kutetea haki za wanyonge na makundi mengine ya kijamii.
“Ndesamburo nimemfahamu muda mrefu, alikuwa mtu makini, alisimamia haki na kutetea wanyonge... kazi aliyoiacha itaendelea kusimama kama maandiko matakatifu yanavyoelekeza, alipigania demokrasia, tusiogope katika kusema kweli,” alisema.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi ambaye alihudhuria katika msiba huo alisisitiza kuwa serikali inathamini mchango wa Ndesamburo katika maendeleo ya taifa ambapo amesema kuwa Ndesamburo alikuwa kiunganishi bila kujali itikadi za vyama.
Kwa upande wake Kiongozi wa Upinzani bungeni na mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alisema kuwa msiba huo ni pengo kubwa sana kwao amesema watakachoweza kukufanya ni kuenzi kazi za Ndesamburo kwa ni alikuwa mpenda haki na mtetezi wa wanyonge.
Alimuomba Waziri Lukuvi ambaye pia ni mbunge awasilishe kwa viongozi wa serikali kuwa wabunge wa chadema siyo wakorofi wala hawana utaratibu wa kugoma bali ni pale tu baadhi ya viongozi wa serikali wanapotoa matamko na hawataki kusikiliza kauli za wengine hatutakaa kimya kwani utakuwa ni unafiki.
Mbali na Waziri Lukuvi, wengine walioshiriki maziko hayo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Juma na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye ambao pia ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho kutoka makao makuu na mikoa mbalimbali.
Dkt.Philemon Ndesamburo alizikwa nyumbani kwake mtaa wa KDC Kata ya Kiboriloni Manispaa ya Moshi, baada ya kufariki ghafla Mei 31, mwaka huu. Alijisikia vibaya akiwa ofisini kwake na alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini,
| Gari lililobeba mwili wa Dkt Philemon Ndesamburo likiingia katika eneo la kanisa la KKKT Usharika wa Kiborloni Moshi Kilimanjaro |
![]() |
| Kaburi alimozikwa Dkt Philemon Ndesamburo |


No comments