Rais aagiza walioshindwa kuendeleza viwanda wakamatwe, wawekwe gerezani,Watanzania walioweka fedha zao nje ya nchi waje wawekeze kwenye viwanda
Na.Vero Ignatus ,Chalinze Pwani.
Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.
Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.
Ameyasema hayo katika siku yake ya mwisho wa
ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambapo alikwenda kuzindua kiwanda
cha Sayona kilichopo Mboga halmashauri ya chalinze ambapo amemuagiza waziri kuwafuatilia wale wote waliouziwa viwanda na
hawajaviendeeza kuwanyang’anya na kuwapa wawekezaji wengine ambao wanaweza
kuviendeleza.
“Viwanda siyo mwanamwali wa kutunzwa ndani ,waziri nakuagiza tumia nguvu katika kufuatilia hili, nataka siku moja uniletee orodha watakaojifanya wajuaji wa kupinga niambie tutatumia hata polisi kuwakamata na kuwasondeka ndani”.alisema Rais.
Kutokana na hilo, Rais amesema; "natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda kipindi cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi mrudishe na wewe Waziri Mwijage tumia hata nguvu kama kuwaweka ndani weka tu siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi."

“Kipindi
cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu
binafsi, sasa kuna viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa
hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.
“Watanzania wote walioweka pesa zao nje ya nchi waje
wawekeze kwenye viwanda hapa nchini kwani wakifa na fedha zao zitakufa vilevile,makosa
tuliyoyafanya ni kuuza viwanda kwa watu ambao wameshindwa kuviendeleza mfano
morogoro kunawatu wanafugia mbuzi kwenye majengo ya vilivyokuwa viwanda ni aibu
kubwa.”alisema

No comments