Shirika la maendeleo ya mitaji la umoja wa Mataifa(UNCDF), limezindua mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa.

Image result for mrisho gambo picha   
Related imageShirika la maendeleo  ya mitaji la umoja wa Mataifa(UNCDF), limezindua  mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la  la hisa kuuza vipande na kutoa hati za dhamana.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amezindua mpango huo jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi za Rais(TAMISEMI) George Simbachawene  na kuwataka watendaji wa halmashauri za majiji na manispaa ,wanaohudhuria mafunzo hayo kujiandaa kutumia fursa hiyo.

Gambo amesema mpango huo unatarajiwa kuongeza mapato kwa halmashauri za majiji na manispaa nchini, kutokana na kuelimishwa ni jinsi gani wataweza kuwekeza katika soko la hisa na kupata fedha za miradi ya maendeleo.

Awali, Mratibu wa mfuko wa mitaji wa umoja wa mataifa(UNCDF) Peter Malika alisema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matano na manispaa tatu.
Related image
Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia, amesema mpango huo tayari umeonesha mafanikio katika majiji kadhaa, ikiwepo Afrika Kusini,  Marekani na Asia na wanatarajiwa utaboresha mapato ya halmashauri.

Kihamia amesema jiji la Arusha tayari limejiandaa kunufaika na mpango huo na tayari lina kampuni ya Arusha Investment ambayo inaweza kushiriki katika masoko ya hisa.

No comments