Simbachawene ahamasisha Teknolojia ya Kilimo Ihamishiwe kwa Wakulima
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene akifungua maonesho
ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya
Themi,Njiro jijini Arusha.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili
kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed
Co kabla ya kufungua
maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja
vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa
kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili
kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed
Co kabla ya kufungua
maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja
vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa
kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(kulia)akipewa
maelezo ya namna ya kulima bila kutumia udongo na Mtalaamu wa kilimo wa
kampuni ya Rijk Zwaan alipotembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni
ya mbegu hiyo kwenye viwanja
vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa
Arusha,Charles Mkumbo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili
kushoto)akiangalia namna kikundi cha Nronga Women Dairy cha wilaya ya
Hai mkoa wa Kilimanjaro kinavyojishughulisha na uuzaji wa maziwa kwenye
banda la halmashauri ya Hai kwenye viwanja
vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Hai,Gelasius Byakanwa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza kwenye maoenesho ya 24 ya wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini .
Nteghenjwa
Hosseah - Arusha
Nane nane ni miongoni
mwa maonyesho maarufu Nchini Tanzania ambayo huwagusa na kuwakutanisha
wakulima, wafugaji, wavuvi wa Mjini na Vijijini, Taasisi za Serikali na binafsi
zinahusika na sekta hiyo zilizopo ndani na nje ya Nchi pamoja na Wadau wa
Kilimo.
Maonyesho ya Nane nane
hutoa fursa kwa wadau wote wa sekta ya Kilimo kuonyesha bidhaa mbalimbali za
Kilimo, kuuza bidhaa hizo, kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia
mbalimbali zia kuboresha Sekta ya Kilimo ili kuondokana na Kilimo cha kufa na
kupona na kuwa Kilimo chenye Tija kinanachofaa kwa biashara na kutosheleza kwa
chakula.
Katika historia ya
maonyesho haya ambayo wakulima kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini hushiriki
ili kujifunza teknolojia hizo mpya za Kilimo kumekuwa na mabadiliko kidogo
katika eneo la utekelezaji wa Teknolojia hizo katika maeneo yao.
Huenda tatizo likawa ni
uelewa mdogo wa wakulima wetu wanaoshiriki katika maonyesho hayo, kutokujifunza
kwa umakini kuhusu mbinu hizo za kisasa au
kukosekana kwa uwezeshaji wa wananchi katika kutekeleza mbinu hizo kwenye maeneo yao au kutokuwa na usimamiza wa maafisa Ugani katika maeneo mengi ya
Kilimo Nchini.
Ushiriki wa mazoea
katika Maonyesho haya unaelekea kufika mwisho baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kufungua
Maonyesho ya 24 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyiika Mkoani Arusha katika viwanja
wa Themi – Njiro.
Wakati wa Ufunguzi wa
Maonyesho hayo Waziri Simbachawene alikagua mabanda mbalimbali ya Kili mo na
Mifugo ya Halmashauri za Kanda ya Kaskazini, Sekta binafsi za Kuzalisha Mbegu
bora, Pembejeo, Zana za Kilimo viwatilifu pamoja na dawa za Mifugo na kujionea
teknolojia bora na za kisasa zinazoweza kumsaidia Mkulima na Mfugaji kuachana
na kilimo cha kujitaftia chakula na kuhamia kwenye biashara njia itakayoweza
kumuo ngezea kipato na kumwinua kiuchumi.
Akifungua Maonyesho
hayo Mhe. Simbachawene amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauro zote Nchini sambamba na Maafisa Ugani
kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye maonyesho haya na kwenda kuwafundisha wananchi na
kuwawezesha kuzitekeleza katika maeneo hayo.
Amesema kuanzia mwaka
huu nataka maonyesho haya yanalete mabadiliko kwa wananchi wetu kwa kuwawezesha
kulima kwa Tija kwa kutumia eneo dogo na kuweza kupata mazao mengi, kufunga
kisasa kwa kuwa na mifugo bora na michache lakini yenye faida kubwa pamoja na
kuanzisha ufugaji bora wa samaki katika maeneo mengi Nchini.
“Kuanzia mwakani
tutaanza kufanya tathmini ya namna ambavyo maonyesho haya yamebadilisha maisha
ya wakulima wetu katika Halmashauri na sio kila mwaka Halmashauri zinashiriki
lakini hamuondoki na kitu kipya wala hamuwasaidii wakulima wa kule vijijini
ambao huenda hawapati fursa ya kuja kuona mapinduzi haya katika Kilimo”.
Akimkaribisha Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho haya
Kanda ya Kaskazini amesema katika mara
hii ya kwanza ambapo maonyesho haya yametoka kwenye Chama cha Wakulima na Wafugaji (TASO) na
kuratibiwa na Serikali wamejitahidi kushirikisha wadau mbalimbali wenye
teknolojia tofauti tofauti ili kuweza kutoa wigo mpana kwa wakulima na wafugaji
kujifunza zaidi.
Pia aliongeza kuwa
ameunda kamati ambayo itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro kuchunguza namna
ambavyo TASO walivyokuwa wanafanya kazi, Mali zinazomilikiwa na Taso, Mapato
yaliyopatikana wakati wa uratibu wao na namna ambavyo yalitumika na mgawanyo wa
kazi zao na kuja na usahuri wa kitaalam juu ya nini kifanyike katika kuboresha
zaidi usimamizi wa maonyesho hayo.
Waziri Simbachawene
amefungua maonyesho haya ikiwa ni ya Pili tangu maadhimisho ya Sherehe hizi
yalipoanza na alifungua Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo – Lindi na atafunga
maoneysho katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.






No comments