SHILIGI MILIONI 500 ZINAHITAJIKA KUZUNGUSHA UZIO BWAWANI SEKONDARI
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwawani wakiwa wanafuatilia jambo katika siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wanafunzi wakionyesha mavazi ya ubunifu waliyoyatengeneza wenyewe shuleni hapo. Picha na Vero Ignatus Blog.
Wanafunzi wakiwa wanaonyesha maigizo mbalimbali yanayohusu utandawazi ukitumiwa vizuri hauna madhara ila ukitumika vibaya unaleta madhara Mamkubwa katika jamii haswa kwa wanafunzi na Vijana. Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika siku hiyo katika Shule y'all Sekondari Bwawani iliyopo mkoa wa Pwani Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mgeni rasmi Kamishna wa Magereza CP Sanga akiwa anazungumza Siku ya wazazi katika Shule ya Sekondari ya Bwawani. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bwawani ACP Emmanuel Lwinga akisoma risala katika siku ya wazazi katika Shule Hiyo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus, Chalinze Pwani.
Shilingi milioni 500 zinahitajika ili kuzungushia uzio katika Shule ya Sekondari Bwawani iliyopo Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani,ikiwa ni majibu ya swali kutoka Kwa mzazi akitaka kufahamu shule hiyo itazungushiwa ukuta yakiwa ni maadhimisho ya 14.
"Itabidi tushauriane hizi pesa zitapatikanaje maana haziwezi kupatikana kwenye ada ya wanafunzi Ada hizo ndizo zinazotumika kuwahudumia kwa chakuka, matibabu na vifaa vya shule. Kwahiyo kutokana na ukubwa wa hii na hizi gharama itabidi tupitishe harambee ,na kama kuna wafadhili mnaowafahamu wanaweza wakatusapoti basi muwasiliane nao"alisema Kamishna huyo.
Amesema kuwa kwa upande wa gari mwenye shule ambae ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza amesema alipanga kuwa shule ipatiwe gari katika gari zitakazonunuliwa kwa matumizi ya jeshi ,hivyo wanasubiria gari hizo zikipatikana mmoja wapo iletwe kwenye shule ikiwa hiyo ni plan A.
"Ikifeli plani( a) tufikirie plan (b) Ile ada tunayolipa kwa mwaka 150,000 iongezwe hapo shilingi 50,000 kwa mwaka tutapata zaidi ya shilingi milioni 30 tunaweza kupata gari zuri tu"alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ACP Immanuel Lwinga amewaambia wazazi watambue kuwa lengo kuu la kuwaleta wanafunzi shuleni hapo ni kupata elimu bila kuacha kuabudu kulingana na imani zao.
"Kimsingi Siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wanafunzi wanaruhusiwa kwenda kuabudu, na kabla ya vipindi vya jioni saa moja kamili huwa tunawaruhusu wanafunzi kwenda kusali kila mtu kwa imani yake kwenye vyumba vya madarasa vinageuka kuwa kama nyumba ya kuabudu"alisema Lwinga.
Aidha amewataka wazazi kufahamu kuwa Taasisi ya elimu Kwanzaa shule ambazo siyo za dini ni vigumu kutenga chumba maalumu kwaajili ya wanafunzi kuswali kwani itamfanya mwanafunzi kuathirika kutokana na yale masaa ya swala ndiyo maana shule imetenga siku kwa kila dhehebu wakasali kulingana na imani yao.
"Shule za dini zikiwemo seminari zinautaratibu wao lakini tukiwa Kama hivi ni ngumu wazazi eleweni " alisisitiza.
Awali risala iliyosomwa na wanafunzi shukeni hapo ilionyesha changamoto mbalimbali ikiwemo ya shule kukosa uzio, gari la kuwapekeka wanafunzi hispitalini nyakati za usiku, upungufu wa waganga na wauguzi, mahabara, vifaa vya michezo, upungufu wa madarasa kulingana na upanuzi wa shule Hoyoo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bwawani wakiwa wanaimba wimbo katika maadhimisho 14 ya siku ya wazazi shuleni happy. Picha name Vero Ignatus Blog.

Wanafunzi wakiwa wanaonyesha maigizo mbalimbali yanayohusu utandawazi ukitumiwa vizuri hauna madhara ila ukitumika vibaya unaleta madhara Mamkubwa katika jamii haswa kwa wanafunzi na Vijana. Picha na Vero Ignatus Blog.









No comments