WAHALIFU 13 WAUAWA NA POLISI KIBITI
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa
Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika
majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la
Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini
ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika
majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha makasha ya
risasi (magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa
yakitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni
Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa
Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus
Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13
ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu
mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika eneo
la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti
ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki 2, pamoja
na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha silaha aina ya
SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu
13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi
katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa
ya Kibiti. Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli
Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi La
Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa
Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka
kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya
risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu.(Picha na Jeshi La Polisi.)
Tarehe
04.08.2017 huko eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya
Mchukwi, Tarafa ya Kibiti, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji,
Jeshi la Polisi lilimkamata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani akiwa
ana majeraha maeneo mbalimbali ya mwili wake akionekana kuwa alikuwa
anaendelea kujitibia mwenyewe kwa njia za kificho. Mtuhumiwa huyu,
alikamatwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelijensia kuhusu yeye
kuhusika na vitendo vya kufadhili, kusaidia, kuhifadhi na kushiriki
uhalifu wa ujambazi maeneo mbalimbali. Mtuhumiwa alipohojiwa kuhusiana
na tuhuma zinazomkabili alikubali na alionyesha dhamira ya kwenda
kuonyesha Ngome yao.
Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00
Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa
akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa
wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu. Baada ya kukaribia
eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo
lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na
risasi sehemu mbalimbali za mwili wake. Kufuatia majibizano hayo, Askari
Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada
zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa
baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na
majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu
imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu @Mtawa
6. Rajabu Thomas @Roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
|
KIELELEZO
|
UTAMBUZI
|
SILAHA, RISASI NA MABOMU
| ||
1.
|
SMG = 5
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
2.
|
Anti Riot Gun 38mm = 2
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
3.
|
SAR = 1
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
|
4.
|
MAGAZINI = 2
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
5.
|
Risasi za SMG 158
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
6.
|
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
|
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
|
7.
|
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
VIELELEZO VINGINE
| ||
8.
|
Pikipiki = 2
|
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
|
9.
|
Vitenge na Nguo mbalimbali
|
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
|
10.
|
Begi = 1
|
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe
|
Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa
vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili
ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya
uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a. Wananchi
wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba
wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa
taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa
mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote
wanalolitilia mashaka.
b. Natoa
wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti
na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea
maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa
zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa
hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri
kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
c. Mamlaka
za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na
Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa
matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata
taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu
maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa
ni lazima watafute matibabu.
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana
kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao
wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa
wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali. Natoa
wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi
wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na
anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo
baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa
ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni
kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea
kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa
Sheria mara moja.
Natoa wito kwa wananchi ambao
wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha
Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Picha za
watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina
ya watuhumiwa hao ni:
i. Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula
Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu
kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana.
Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo
yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.
Imetolewa na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017





No comments