WANAFUNZI WA LUCKY VICENTI KUREJEA NYUMBANI KESHO IJUMAA
Pichani ni watoto Sadia,Doreen na Wilson pamoja na mama zao ,(aliyevaa suti) ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Wilson Masilingi wakiwa sioux City Lowa nchini Marekani.Wanatarahiwa kurejea nchini siku ya ijumaa asubuhi.
Na.Vero Ignatus,Arusha
Na.Vero Ignatus,Arusha
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwaongoza Watanzania kuwapokea majeruhi (3)wa
ajali wa Shule ya Lucky Visent katika uwanja wa kimataifa wa KIA siku ya ijumaa
wakitokea nchini Marekani majira ya saa tatu asubuhi kwa ndege aina ya DC -8 namba SP
ambayo imetolewa na shirika la The Samaritan Purse kutoka mji mkuu Shaloth North
Carolina na watakuwa angani kwa masaa
18.
Akizungumzia
ujio wa wanafunzi hao Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amewaomba
wazazi ndugugu jamaa na marafiki wanaopenda kuwapokea watoto hao wawahi
uwanjani saa amesema kuwa ujumbe wa baraza la congress ukiongozwa na ujumbe wa
baraza Man Stive King pamoja na wageni
mbalimbali watawasili Kilimanjaro saa
moja kamili asubuhi siku ya ijumaa
Aidhaa
amesema kuwa watoto Doreen, Sadia na
Wilson wapo tayari kurejea nyumbani ,amewaomba watanzania wajumuike pamoja
kuwapokea watoto hawa .ambao walipelekwa marekani mei 14 kwaajili ya matibabu yaliyoratibiwa na Stemm kwa kushirikiana na shirika la ndege la Samaritan Purse linaloongozwa na mchungaji Franklin Graham wa nchini Marekani
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mbunge huyo ambae tangia watoto hao wasafirishwe amekuwa akitoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii facebook amesema kuwa ndege itakayowarudisha watoto hao pamoja na mama zao na daktari bingwa Elias Mashalla na muuguzi kutoka hospitali ya Mount Meru itawasili ijumaa asubuhi.
Ikumbukwe kuwa watoto hao ni manusura wa ajali iliyotokea mei 6/ 2017 ambapo wenzao 32 walipoteza maisha ,walimu 2 na dereva mmoja ,wao walisafirishwa kuelekea nchini Marekani na Shirika la Samaritan Purse kwaajili ya matibabu.

No comments