WATANZANIA WAASWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI YA NCHI
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Wito
umetolewa kwa Watanzania watumie bidhaa za ndani zaidi kuliko kuzipa kipaumbele
bidhaa za nje ya nchi kwani wazalishaji wa ndani wanazalisha bidhaa zenye ubora
zaidi.
Hayo
yamesemwa na mzalishaji wa bidhaa zitokananzo na maziwa kutoka kwenye kampuni
ya The Grand Demam iliyopo jijini
Arusha Omari Cuba ambapo wameiomba serikali wapunguze kodi kwa
wasindikaji wa ndani kwani ni kubwa ukilinganisha na wale wanaoingiza bidhaa
kutoka nje ya nchi.
Amesema kuwa
changamoto kubwa waliyo nayo kama wazalishaji ni ushindani wa bei,bidhaa za
ndani zinakuwa na bei ya juu zaidi kuliko bidhaa zinazotoka nje ya nchi,hivyo
basi wameiomba serikali kuwatupia macho wajasiriyamali wa ndani zaidi.
Pia ametoa
ushauri kwa wananchi wasitumie maziwa ambayo hayajafanyiwa usindikaji kwani
hayana usalama yanakuwa na vyanzo vya magonjwa,au la yakiwa hayajasindikwa wahakikishe
kuwa maziwa yanachemshwa kwa kiwango kinachotakiwa kwa matumizi ya kibinadamu.
“Ukiwa
umekunywa maziwa ambayo hayajachemshwa unakunywa bacteria walio hai, unakuwa
umepanda katika mwili wako maradhi ambayo yatakuja kuibuka hapo baadae”alisema
Omar.
Sambamba na
hayo wameiomba serikali ifanye matangazo lau mara mbili kwa mwezi kwa njia ya
radio,Luninga na mitandao ya kijamii ili kufanya uhamasishaji kwa wananchi waweze
kutumia maziwa pamoja na bidhaa zitokanazo na maziwa.
No comments