WANAFUNZI WA LUCKY VICENT WARUDI NYUMBANI SALAMA




Ndege ya Samaritan Purse iliyowabeba watoto WA Lucky Vicent ikiwa imeshatua Katika Kiwanja cha Kimataifa cha KIA.Picha na Vero Ignatus Blog


 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisalimiana na mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.Picha na Vero Ignatus Blog.


Wakwanza kulia ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa na vazi tayari kuelekea kwenye ndege kuwapokea watoto. Picha naVero Ignatus Blog 


Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu akiwa amevaa vazi husika kwaajili ya kuingia kwenye ndege kuwasalimu watoto. Picha na Vero Ignatus Blog.



Watoto Shadia,Wilson pamoja na Doreen wakiwa wameshashuka kwenye ndege wakielekea sehemu maalum iliyotengwa kwaajili yao. Picha na Vero Ignatus Blog.

 
Wanafunzi wa Lucky Vicent wakiingia katika Kiwanja cha Kimataifa cha ndege Kia kwaajili ya kuwapokea wenzao ambao walikuwa Marekani kwa matibabu.Picha na Vero Ignatus Blog.




Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa amemaliza kusoma hotuba ambayo alimuwakilisha makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,pembeni ni Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiwa ameshika karatasi.



Na.Vero Ignatus Arusha

SERIKALI imewanya Madaktari na Wauguzi wasio na uzalendo na ubadhirifu wa dawa za hospitalini waache kufanya hivyo ili kuokoa maisha ya wagonjwa.

Hayo yamesemwa na mkuu  mkoa wa  Kilimanjaro Anna Mghwira Katina Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  (KIA) kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema inaita uchungu kuona watoto hao watatu wamekwenda  Marekani kutibiwa kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu na ubadhirifu wa Mali za umma.

"Inatia uchungu  sana kuona watoto hawa Doreen Mshana, Wilson Tarimo na Sadya Awadhi wangeweza kutibiwa hapa Kama wauguzi na madaktari wasingekuwa wabadhirifu,"alisema hotuba hiyo huku akilia

Aidha imemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kukabidhi fedha zilizobaki za rambirambi Sh.milioni 20 kwenye Mfuko maalum wa Tanzania Miracle Children Foundation ulioanzishwa na Shirika la Stemm  ajili ya kusomesha watoto watatu waliopata ajali hadi Elimu ya chuo kikuu mahali lolote Duniani watakakosoma.

Aidha alishukuru Madaktari wa Marekani na serikali yao mbali na kuwarudhisha salama watoto hao wameleta vifaa vya kusaidia hospitali hizo.

Pia alikabidhi hati maalum ya utambuzi wa mchango wa kuokoa maisha ya hao watoto kwa Lazaro Nyalando, Steve King Mjumbe wa Bunge la Marekani na Dk.Steve Meyer Ambaye Dk .bingwa wa mifupa aliyeongoza jopo la madaktari waliotibu watoto hao na Mkurugenzi mwenza wa Shirika la Stemm linalodhaminiwa na Samaritan's Purse

Alisema mungu akawafanye kuwa njia na mfano kwa watumishi wabadhirifu nchini na wakatimize ndoto zao.

Naye Mratibu Mkuu wa zoezi la watoto hao kwenda Marekani, Lazaro Nyalandu alisema ni u pendo wa familiya yake Rais John Magufuli ambaye aliendesha  upatikanaji wa Visa Ubalozi wa Marekani siku ya Jumapili.

"Haikuwa Rais Ubalozi tutoe Visa jumapili na yalibaki mass a Matson Ndege ilitakiwa kuondoka nchini, lakini Rais Magufuli aliwezesha jambo hilo kuwa rais hivyo mungu ambariki na serikali yake,"alisema.

Alisema Tanzania na watu wote no vema kumshukuru mungu kwa uponyaji alipenda kwa watoto hao na kuwavusha katika mtihani mkubwa katika maisha yao.

DK.Bingwa wa mifupa wa hospitali ya Mkoa Mount Meru Elias Mashalla alisema anasikia raha kurejea nchini akiwa na watoto hao wakitembea licha ya kuondoka nao wakiwa katika machela.

Kwa upande wake Dk.Steve Meyer kiongozi wa jopo la Madaktari, alisema mungu ametenda muujiza wa uponyaji watoto hao.

Alisema licha ya kuwarudisha salama wameleta na vifaa mbalimbali vya kumsaidia hospitali nchini kusaidia matibabu kwa wagonjwa.

"Licha ya sisi kuwa madaktari bingwa wa mifupa lakini mungu ametenda muujiza kuwaponya watoto hawa kwa ajili ya kuonyesha ukuu wa mungu,"alisema

Kwa upande wake Mjumbe wa Bunge la Marekani,Steve King alisema alipigiwa simu na Mkuu wa Samaritan's Pass Bill Graham kamwomba msaada wa kizungumza na serikali ya Marekani ili kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania kupata Visa kwenda Marekani katika matibabu.

"Nilipopata huu ujumbe nilianza kuwasiliana na uongozi wa Marekani na Ubalozi wa Tanzania wa Marekani na kufanikisha kuwabana watoto hawa,"alisema

Watoto Doreen Mshana,Wilson Tarimo na Sadya Awadhi walishukuru serikali,viongozi,Madaktari,Wauguzi na watanzania kuwasaidia hadi kurejea katika afya njema.

Katika mapokezi hayo walishiriki viongozi wa dini ambao ni Askofu Eliud Isangya wa Kanisa la kimataifa la Evanglism na Shelve Mkuu wa Mkoa wa Arusha Shaban Juma na kuongeza sala ya kumshukuru mungu kwa muujiza wa uponyaji.

PIA viongozi mbalimbali wa kisiasa, wanafunzi wa shule yao Lucky Vicent na wananchi walijumuika uwanjani hapo kuwapokea huku baadhi yao walitokea na machozi kwa furaha.

No comments