DAWASCO WAZINDUA HUDUMA YA MAJI MTANDAONI HABARI24 TV 10:32:00 PM
Na Mwandishi wetu,
Shirika
la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limezindua mfumo mpya
wa Mawasiliano ambao unalenga kumrahisisha mteja kupata na kutoa
taharifa.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano
na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo la mfumo huu ni
kumuweka mteja karibu kihuduma.
"Smartphone
itamuwezesha kila mwananchi kupakua huduma hii hili aweze kupata huduma
kwa kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO Ambapo baada
ya kufuata hatua zote za kujisajiri mteja atatumiwa neno la Siri"
amesema Kingu.
Naye,
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi
wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na
hauna gharama zozote.
Anasema
ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu
huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja
alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya
maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.
“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika
simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama
zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote
muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na
ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.
Amesema
kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa
kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka
taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akionyesha mfumo
wa Huduma Mtandaoni unavyofanya kupitia simu za mkononi
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akifafanua jambo
kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika
simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika
hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting
Lyaro.
Meneja
Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, akizungumza na Waandishi wa
Habari wakati wa Mkutano wa kuzindua huduma ya simu mtandaoni
Waandishiwa habari waliohudhuria mkutano huo
No comments