Zaidi watu 250 wameuawa kwenye maporomoko ya ardhi Sierra Leone

A picture of the mudslideMaporomoko ya ardhi yafukia watu wengi Sierra Leone 

 Idadi ya watu waliouwa kwnye maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone haujulikani baada ya idaia tofauti kutolewa.

Shirika la habari la AP linasema kuwa takriban watu 250 wameuawa.
Eneo moja la milima liliporomoka mapema leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa kwa mjibu wa mwandishi wa habari wa BBC Umaru Fofana

Makamu wa rais nchini Sierra Leone Victor Bockarie Foh, alisema kuwa kuna uwezekano kuwa mamia ya watu wameuawa akiongeza kwa idadi ya watu waliouawa huenda ikaongezeka.
Mwandishi wa habari aliye eneo hilo anasema kuwa watu wemgi walipatwa wakiwa bado wamelala wakati maporomoko yalitokea
Mafuriko yamekuwa makubwa
Mafuriko yamekuwa makubwa
"Mke wangu amekufa, watoto wangu wote wamekufa, Leo asubuhi niliongea na watoto wangu kabla ya kuenda kazini. Mmoja wao hata alinipa soksi nilizovaa." alisema mwathiriwa mmoja.

"Tulikuwa ndani, tukasikia udongo ukikaribia, tukajaribu kukimbia, nilijaribu kumchukua mtoto wangu, lakini udongo ulikuja kwa haraka sana . Alifukiwa akiwa hai. Sijamuona mume wangu. Mtoto wangu alikuwa na umri wa wiki saba." alisema muathiriwa mwingine.
Mafuriko yamekuwa makubwa
Mafuriko yamekuwa makubwa
Maafisa wanasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi kamili ya watu waliouawa
Watu wamesambaza picha za uharibifu uliotokea kwenye mtandao wa twitter ya za mafuriko ndani nanje ya mji wa Free town.
 Sierra Leone
  Sierra Leone 
 
 
chanzo bbc 

No comments