Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna
Abdallah (katikati) akiwa na Girl Guides waliorejea nchini kutoka kwenye
programu ya Yess ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya uongozi,
utamaduni na maadili katika nchi za Uganda, Madagascar, Zimbabwe na
Zambia.
Hapo
ilikuwa wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa na TGGA Dar es Salaam kwa
ajili ya kuwapongeza na kupata mrejesho wa walichojifunza walipokuwa
kwenye programu hiyo inayodhaminiwa na Norwey.Anna Abdallah aliwapongeza
wasichana hao wanne kwa kuiwakilisha vizuri TGGA na Tanzania katika
programu hiyo nje ya nchi.
Kutoka kulia ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Farida Mjoge aliyekuwa Uganda, Elizabeth Betha (Madagascar) na Edna Chembele (Zimbabwe)
Girl
Guides hao wakipata msosi wakati wahafla ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay,
Dar es Salaam.
Anna
Abdallah akiotoa nasaha na pongezi kwa Girl Guides kwa kuiwakilisha
vizuri TGGA NA Tganzania kwa ujumla, ambapo aliwataka watumie mafunzo
waliyoyapata kwa kutoa mafunzo kwa wasichana wenzao nchini.
Wakiwa na furahani Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), Anna Abdallah (katikati) na Mjumbe wa TGGA, Agnes Makenya
Katibu
Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba akitoa neno la ukaribisho muda mfupi
kabla ya Girl Guides waliorejea nchini kutoka nje ya nchi kwenye
programu hiyo kuelezea mambo mbalimbali waliyoyafanya na kujifunza
Grace Shaba akiwatambulisha Girl Guides hao
Ummy Mwabondo akielezea kwa njia ya picha kazi mbalimbali alizokuwa anazifanya alipokuwa Zambia
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema
akitoa ufafanuzi wakati Girl Guides wakielezea mafanikio na changamoto
ya mafunzo yao nje ya nchi
Girl Guides Farida akielezea mambo mbalimbali aliyoyafanya akiwa Uganda kwa muda wa miezi sita.
Viongozi na wageni waalikwa wakionesha ishara ya TGGA
Viongozi wa Girl Guides Makao Makuu ya TGGA wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), akiwa na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA wakijadili jambo
Sasa ni wakati wa msosi
Mwenyekiti
wa TGGA, Profesa Martha Qorro akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdala kuzungumza katika
hafla hiyo.
Mwakilishi
wa wazazi wa Girl Guides hao, Florence Gondwe akitoa shukrani kwa TGGA
kwa kuwapatia wasichana hao fursa ya kwenda nje ya nchi kwenye programu
hiyo ambayo alidai itawasaidia sana kimaisha.
Kamishna Hangi akitoa neno la shukrani kwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo pamoja na Girl Guides
Wakiwa katika picha ya pamoja
Anna Abdallah akiagana na Girl Guides baada ya hafla kumalizika
No comments