NDEGE 5HSAL 206 YAPATA AJALI YAUA MMOJA MONDULI

Ndege yenye namba 5HSAL 206 ambayo inayomilikiwa na
kampuni ya Safari Air Link kama inavyoonekana ilipoangukia katika hilo limetokea katika kijiji cha Engalaoni kilichopo katika mpaka
wa wilaya za Monduli na Arumeru za mkoani hapa.
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Mtu mmoja mkazi wa jijini Dar Es Salaam, David Mbale(25),ambae ni Rubani amefariki dunia
baada ya ndege ndogo aliyokuwa akiendesha kuanguka juu ya vilima vya
Monduli.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema kuwa
tukio hilo limetokea katika kijiji cha Engalaoni kilichopo katika mpaka
wa wilaya za Monduli na Arumeru za mkoani hapa.
Amesema
kuwa tukio hilo lilitokea juzi Agosti 9,ambapo marehemu alikuwa
akiendesha ndege ndogo yenye namba 5HSAL 206 ambayo inayomilikiwa na
kampuni ya Safari Air Link.
Alisema
kuwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria watano iliondoka katika
uwanja mdogo wa ndege wa Arusha,majira ya saa 1;30 asubuhi ambayo
ilikuwa ikielekea katika eneo la Kogatende,Serengeti kuwachukua watalii.
"Ndege
hiyo alikuwepo rubani peke yake na alikuwa anasubiriwa Serengeti na
watalii jambo ambalo lilifanya taarifa zilianza kuenea saa 4 asubuhi kuwa ndege hiyo
imeanguka katika vilima vya Monduli maarufu kama Monduli Hills,"alisema
na kuongeza
"Mara baada
ya taarifa hizo kutolewa saa 6;30 tulipozipata taarifa hizo tulijulisha
kikosi cha zima moto na wenzetu wa uwanja wa ndege wa Arusha,na
walipofika kwenye kilima hicho walikuta rubani ameshafariki dunia,mwili
ulichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi,"
Amesema
kuwa uchunguzi wa tukio hilo umeanza jana na kuwa watashirikisha
wataalamu ambao wamebobea katika masuala hayo kutoka kwa wataalamu
wanaoshughulikia masuala ya ndege wakishirikiana na maafisa wa jeshi
hilo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

No comments