MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio
mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo
siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga
mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya
asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba
atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya
Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.
Katika
Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya
Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa
Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna
nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.
Makamu
wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani
michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo
Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi

Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kusokota kamba
Vijana kutoka Kusini mwa Kizimkazi wakivuta kamba wakishindana na vijana wa kaskazini wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye
uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Bw. Sudi Simba ambaye alifika Kizimkazi kutambulisha
huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya
Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya
Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia vipeperushi vyenye taarifa ya huduma ya bima ya Afya ya Afya
Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja
wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Wakazi wa Kizimkazi wakiangalia ngalawa 15 zikichuznz vikali ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi
Wananchi
wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed
Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana
aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khamisi Mgeni akiwa na
chombo chenye jina la Sea Never Dry.






No comments