TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA YATOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA KUPELEKA VYAKULA KUPIMWA KUHAKUKI VIASILI VYA MIONZI

Wakwanza kushoto ni Afisa uhusiano kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Peter Ngamilo akiwa anatoa elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Njiro mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.

Agrey kitosi mwandisi wa mionzi kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki mkoani Arusha akitoa elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini.Picha na Vero Ignatus Blog.

Mwanasayansi wa mionziDenis mwalongo akizungumza na mgeni aliyetembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha


Umati wa wananchi waliofurika katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini kama wanavyoonekana pichani .Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus. Arusha
Wito umetolewa kwa kwa waanyabiashara ,Wakulima na wafugaji waendelee kutoa ushirikiano wa kuhakikisha kwamba wanatoa sampuli zao za vyakula /bidhaa kwenye Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania kwaaajili ya uhakiki wa viasilia vya mionzi ili kuweza kuwalinda watanzania na madhara yatokanayo na mionzi
Hayo yamesemwa na Afisa mahusiano mwandamizi kutoka tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo mkoani Arusha ambapo amesema kuwa Tume hiyo inajihusisha na udhibiti wa vyanzo vya mionzi kuhamasisha matumizi salama teknolojia ya nyuklia
Amesema kuwa lengo la kushiriki maonyesho ya nanenane
Kutoa elimu kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa za vyakula nje ya nchi au kuingiza bidhaa za mazao ya kilimo ndani ya nchi kwani kazi yao kubwa ni kuangalia vimelea vyote vya mionzi kwenye chakula.
Ngamilo amesema kuwa mwitikio
wa wakulima na wafugaji ni mkubwa mara baadaya kupata elimu wengine
walikuwa wagumu kuleta sampuli za vyakula ili vipimwe mara baada ya
kupata elimu wameleta sampuli za vyakula ili vikapimwe
"Miaka ya nyuma tulikuwa tunapata taabu sana pale unapomuelewesha mkulima au mfugaji kuhusiana na kuleta sampuli za vyakula kwenye Tume ili vikapimwe ila tunashukuru baada ya kupata elimu wakulima wenyewe wamekuwa wakileta sampuli ili zikzpimwe"alisema
Wamita kupata elimu juu ya upimaji wa sampuli tofauti na miaka mingine
Kwa upande wake Mwanasayansi wa mionzi Denisi Mwalongo amesema kuwa jukumu kubwa la tume ni kulinda wananchi dhidhi ya madara yanayoweza kusababishwa na mionzi huku akiainisha aina kuu mbili za mionzi ambayo ni Miaonzi ayonishi na Mionzi isiyoayonisha .
"Mionzi isiyoayonisha ni mionzi ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu mfano xray gamareys,
Isiyoayonisha ni kama mionzi ya simu radio"Alisema.
Nchi zaidi 152 duaniani wanachama wa tume za nguvu za atomiki duniani
Hadi
sasa hawajaweza kubaini nguvu za mionzi katika vyakula vinavyoingia
kutokana na ushirikiano walionao katika utendaji kwani vyakula vikitoka
nje vinapimwa vikiingia vinapimwa pia mionzi iliyopo ni ya kawaida
haijavuka hadi kuonekana ni hatari kwa mwanadamu
"Mionzi inaweza kusababisha ukemia au kansa
Ukitumia
muda mrefu sana kuongea na simu kwa muda mrefu,kukaa kwenye kompyuta
muda mrefu,kuhifadhi simu katika maeneo hatarishi katika baadhi ya
sehemu za mwili kwasababu miili yetu ni tishu inazalisha mionzi kwa
haraka sana"
.
No comments